Na Silvia Mchuruza,Kyerwa – Kagera.
Waziri wa madini Dotto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini ya bati (TIN) mkoani kagera wilayani kyerwa kuwa wavumilivyu kwa kipindi hiki ambacho machimbo ya madini hayo yamefungwa kutokana na muwekezaji kuacha kununua madini.
Ameyasema hayo wakati alipowatembelea wachimbaji wadogo na kuweza kujionea hali harisi iliyopo kwa kufanya ukaguzi wa maeneo ya machimbo hayo huku akiwataka wachimbaji hao kuwa wavumilivu kwa kukosa soko la kuuza madini hayo .
Hata hivyo ameongeza kwa kusema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi kwa wachimbaji amewataka kuacha kutorosha madini hayo hata kama nchi aina uwezo wa kupata soko zuri na kusema kuwa wachimbaji hao waache kukuza masoko ya nje na teknolojia ya nje na badala yake wakuze teknolojia ya nchi ya Tanzania.
“tunajua soko kwa sasa ni gumu lakini tuache kulaumiana maana hapo mwanzo bei ya madini haya ilikuwa chini ila sasa imeongezeka kilichopo tuache kujadili majungu bali tujadili pesa tujue ni vipi tutaweza kurudisha biashara katika eneo hili kutokana na watu zaidi ya elfu 4 kupoteza ajira zao ndogondogo kutokana na machimbo haya kufungwa”
Aidha nae mwenyekiti wa wachimbaji bwana Osward Inyas kwa niaba ya wachimbaji wenzake akaeleza kukosa mahali pa kuuza tin yao huku wakisema zaidi ya tani 20 zimewekwa stoo kwa kukosa mnunuzi pamoja na kushuka kwa bei ya tin kutoka kati ya 25,000/= na 22,000 hadi elfu 13,000/= kwa kilo moja aliyokuwa ananunulia aliepewa dhamana ya kununulia TANZAPLUS.
“changamoto tunazo za kutosha sana lakini kwakuwa wazili amekuja naamini tutapata muafaka wetu kutokana mnunuzi kuacha kununua miezi saba sasa imepita na kusababisha ajira zaidi ya 4000 kusimama hapo tukiwajumuisha wakuna mama lishe, wachota maji, na vibarua wa kuchimba, huku zaidi ya leserni 250 kuacha kufanya kazi na kubaki leseni 4 tu”
Vilevile wachimbaji hao wakaomba ombi kwa waziri Biteko kwa kumtaka muwekezaji ambae ni TANZAPLUS kwakuwa ameshindwa kununua tin kwa sasa basdi serikali ilwaruhusu kuuza madini yaa kwa kulipa mrahaba kwa mujibu wa sheria na kanuni zake.
Hata hivyo waziri biteko akazidi kuwatia moyo wachimbaji hao kwa kusema kuwa mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa mwezi wa tisa kampuni ya serikali ya madini STAMICO itaungana na muwekezaji huyo ili kuanza kununua madini hayo hili kuwaondolea adha ya kukosa soko la madini ya TIN ndani ya nchi.
Sambamba na hayo akawataka wachimbaji hao kupendana na kupeana thamani na kumthamini muwekezaji huyo kwa maana amefanya mambo mengi nchini ikiwemo na kuchenjua madini hayo na kuyauza nje ya chi zaidi ya tani 3 kwa mara ya kwanza na mara ya pili tani 6 na kuwataka kuacha kurahumu bali waangalie chanzo cha watu hao kuacha kununa madini hayo.