Mkuu wa Mkoa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti akikagua timu kabla ya mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya JPM BODA BODA CUP 2020 katika uwanja wa shule ya msingi Kashai Manispaa ya Bukoba. Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akikabidhi jezi kwa moja ya timu kabla ya kuanza mashindano ya JPM BODA BODA CUP 2020. Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akionyesha uwezo wake wa kucheza soka kwa kupiga dalizi na danadana kabla ya mtanange kuanza.Baadhi ya waendesha pikipiki maarufu BODA BODA wakiwa kwenye maandamano ya kuashiria kuanza rasmi kwa mashindano ya JPM BODA BODA CUP 2020 mkoani Kagera.
********************************
Na Allawi Kaboyo Bukoba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Erisha Gaguti amezindua mashindano ya mpira wa miguu ambayo yatawashirikisha waendesha pikipiki maarufu BODA BODA yatakayozijumuisha timu 18 kutoka Halmashauri 6 za mkoa huo.
Gaguti ameeleza lengo la mashindano hayo kuwa ni kuwaweka vijana hao pamoja na kuwapa elimu juu ya ujasiliamali, elimu ya usalama Barabarani pamoja na elimu ya ulinzi na usalama ili vijana kwa wingi wao waweze kushiriki katika suala zima la kutunza amani kwani wanakutana na wananchi mbalimbali wenye taarifa nyingi.
Ameongeza kuwa vija wa BODA BODA ni muhimu sana kwenye jamii hasa kwenye usafirishaji lakini pia katika suala zima la kulinda amani maana hutumika pia baadhi yao kuwasafirisha wahalifu.
“Tumewaka mashindano haya mahususi kabisa ili kuwafanya vijana kuwa pamoja ili kuweza kuwajengea uwezo wa ujasiliamali maana kazi hii ya usafirishaji ina mwisho wake lakini mtu akiwezeshwa katika njia nyingine ataweza pia kujiendeleza kimaisha na kiuchumi.” Ameeleza mkuu wa mkoa Gaguti.
Mashindano hayo yanazihusisha kata 14 za manispaa ya Bukoba na timu nyingine kutoka halmashauri ya wilaya Muleba, Karagwe, Missenyi na halmashauri ya wilaya Bukoba na mchezo wa ufunguzi umezikutanisha timu za Kata ya Kashai na Bilele.
Aidha amesema kuwa nje mchezo wa mpira wa miguu yatahusisha mashindano ya vipaji ya uimbaji kwa wasanii wa mkoa huu ambapo nao pia watapata zawadi zao.
Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atapa kitita cha shilingi milioni 3.5, mshindi wa pili shilingi Milioni 2.5 na mshindi wa tatu shilingi milioni 2.