Uzinduzi wa promosheni ya TECNO Vimba Season umefanyika rasmi jana huku hafla hiyo ikihudhuriwa na wasanii maarufu wa tamthiliya ya HUBA ambayo huoneshwa na king’amuzi cha Dstv.
Promosheni hiyo ya ‘Vimba Season’ inalenga kuwapatia wateja wa TECNO CAMON15 na Spark5 zawadi mbalimbali ikiwemo seti ya king’amuzi cha Dstv kilicholipiwa chaneli za kifurushi cha familia kwa mwezi mzima, pia wateja wa simu hizi watapata nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye droo ya shindano la zawadi kubwa ya gari.
Wasanii wa tamthiliya ya Huba waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Promosheni ya TECNO Vimba Season jana Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana wakati wa hafla ya uzinduzi huo, meneja mauzo wa TECNO Bi. Mariam Mohamed alisema promosheni hiyo ni mwendelezo wa promosheni ya Vimba Season ambayo hufanyika mara moja kila mwaka.
“Leo kwa mara nyingine tena tumewaletea msimu wa promosheni ya Vimba Season na kwa mwaka huu simu ambazo zitaambatana na zawadi ni TECNO CAMON 15 na Spark5. Kwahiyo Mteja yeyote atakayenunua CAMON15 au Spark 5 ana uwezo wa kuingia moja kwa moja kwenye droo yetu kubwa ya kushinda gari” alisema Bi. Mariam.
Meneja mauzo wa kampuni ya simu ya TECNO akiwa ameshika TECNO CAMON 15 na Spark 5 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jana Jijini Dar es Salaam
Bi Mariam aliongeza kuwa, “Pia tumeshirikiana na Dstv kwa mara nyingine tena, kwahiyo ukinunua simu hizi CAMON15 au Spark5 unapata Dstv na promosheni yetu inaanza rasmi leo nchi nzima”.
Picha ya pamoja ikimwonesha pia msanii wa vichekesho maarufu Pierre Liquid (Mwenye tisheti mbele katikati).
Kwa upande wake meneja masoko wa TECNO Bw. William Motta alisema kuwa promosheni hiyo itafanyika kwa muda wa mwezi mzima nchini kote katika maduka ya TECNO na kuwaomba wateja wote wa TECNO na watanzania kwa ujumla kutoikosa kwani ni fursa kwa kila mmoja.
Kwa taarifa zaidi tembelea: https://bit.ly/2XsrPWm