Meneja Mkuu wa kadi na teknolojia za kidijitali wa BancABC, Bwana Lameck Mushi (kushoto) akionyesha kadi mpya za malipo ya VISA maarufu kama ‘Gusa ulipe’ zinazowawezesha wateja kufanya malipo kwa urahisi, haraka na usalama. Teknolojia hiyo ni ya kisasa zaidi katika kufanya malipo na ni salama na ya uhakika kwa watumiaji.Kulia ni Meneja wa Huduma za uwakala wa benki na mahusiano ya kimkakati wa benki hiyo, Ndugu, Mwita Rhobi. Meneja Mkuu wa kadi na teknolojia za kidijitali wa BancABC, Bwana Lameck Mushi (kushoto) akitoa maelekezo juu ya namna ya kufanya malipo kwa kutumia kadi mpya za malipo ya VISA maarufu kama ‘Gusa ulipe’ zinazowawezesha wateja kufanya malipo kwa urahisi, haraka na usalama. Kulia ni Meneja wa Huduma za uwakala wa benki na mahusiano ya kimkakati wa benki hiyo, Ndugu, Mwita Rhobi. Meneja Mkuu wa kadi na teknolojia za kidijitali wa BancABC, Bwana Lameck Mushi (kushoto) pamoja na Meneja wa Huduma za uwakala wa benki na mahusiano ya kimkakati wa benki hiyo, Mwita Rhobi wakifurahia kuzindua kadi mpya za malipo ya VISA maarufu kama ‘Gusa ulipe’ zinazowawezesha wateja kufanya malipo kwa urahisi, haraka na usalama.
**********************************
Kadi hizo zinatumia teknolojia ya kisasa zaidi ya malipo duniani ambayo inamuwezesha mtumiaji kufanya malipo kwa haraka zaidi katika mashine za POS kwa kugusa bila kuingiza kadi ndani ya mashine ya malipo (POS)
Dar es Salaam. Agosti 5, 2020. Katika kuongeza ubora wa huduma za kadi, BancABC leo imezindua kadi mpya za malipo maarufu kama ‘Gusa ulipe’ ili kuwawezesha wateja wake kufanya malipo kwa urahisi, haraka na usalama. Teknolojia hiyo ni ya kisasa zaidi katika kufanya malipo na ni salama na ya uhakika kwa watumiaji.
Teknolojia hii inaleta mageuzi makubwa kwenye huduma za malipo kwani kwa sasa wateja wataweza kufanya malipo kwa urahisi zaidi kwa kugusisha kadi kwenye mashine ya POS tofauti na ile ya awali ya kuchanja (swipe) au kuchomeka kadi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Meneja Mkuu wa kadi na teknolojia za kidijitali wa benki hiyo, Bwana Lameck Mushi alisema kadi hizo zitaleta urahisi wa malipo kwa kadi kwa wateja na kupelekea uharaka wakati wa kufanya miamala hivyo kuboresha huduma za malipo kwa njia ya kadi.
“Kadi hizi za VISA zinatumia mfumo unaokuwezesha kufanya malipo ya haraka mahala popote na inaondoa ulazima wa kutembea na pesa taslimu ili kulipia huduma mbalimbali. Teknolojia hii inaongeza ufanisi wa malipo kwa wateja wetu kwa sababu mchakato wake ni rahisi na salama zaidi,” alisema bwana Mushi.
Mushi aliendelea kueleza kuwa, miamala itakayofanywa kwa kutumia teknolojia mpya ya gusa ulipe, ina usalama asilimia 100 dhidi ya uhalifu wa mitandaoni kwani bado inatumia ulinzi wa namba ya siri ya mteja (PIN) hususani kwa miamala ya malipo yenye thamani kubwa.
Kwa upande wake, Meneja wa Huduma za uwakala wa benki na mahusiano ya kimkakati wa benki hiyo, Ndugu, Mwita Rhobi alisema “Mbali na kumuwezesha mteja kufanya malipo mtandaoni au kupitia mashine za POS BURE, kadi hizi zinaweza kutumika kwenye ATM zaidi 2,000 zinazopokea kadi ya VISA Tanzania. Pia, inaweza kutumika kwenye ATM zaidi ya milioni 2.7 zinazopokea kadi za VISA duniani na kupitia vituo zaidi ya 24,000 Tanzania vinavyopokea malipo ya kadi za VISA”
Mwita aliongezea kuwa, Kadi hizi zenye teknolojia ya gusa ulipe zinapatikana katika sarafu sita ikiwamo Shilingi ya Tanzania, Dola za Kimarekani, Randi ya Afrika Kusini, Euro, Pauni ya Uingereza pamoja na Yuan ya China.
Mteja anaweza kupata kadi hii kupitia matawi yetu au mtandao wa mawakala wa BancABC zaidi ya 350 waliopo Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Mwanza.
Mteja ataweza kuweka pesa kupitia matawi yetu, na kadi ya shilingi za Tanzania inaweza kuwekwa pesa kwa kuhamisha pesa kutoka mitandao ya simu kama (Mpesa, Tigopesa, Airtelmoney, T-Pesa, Halopesa, EzyPesa) au kupitia mawakala wetu.
Endapo kadi itapotea, kuibiwa au kuisha muda wake wa matumizi, mteja ataweza kupata kadi nyingine kwa kutembelea matawi yetu au kwa kupitia mawakala wetu walio karibu yake. Pia, mteja anaweza kupiga simu namba 0779111000 au 0800714141 kwa huduma ya kuletewa kadi.