……………………………………………………
Na mwandishi wetu Arusha
CHAMA Cha Mapinduzi Arusha Mjini kina watia nia 81 ambao wanaomba
kuteuliwa kugombea ubunge,hata hivyo kumeibukamalalamiko toka kwa
baadhi yao kuanza kurushiana shutuma kali kuwa kuna mgombea ambaye
alitumia mbinu chafu kuweza kupata kura nyingi .
Kutokana na malalamiko hayo na baadhi yao wameandika barua za
malalamiko wakipinga matokeo hayo kwa sababu mbali mbali,wakidai kuwa
kulikuwa na vitendo vya rushwa na taratibu za upigaji kura za
kukiukwa.
Kwa hali ilivyo ni wazi kuwa CCM ina wakati mgumu sana kuweza
kuachana matokeo ya kura za maoni na kuja na mgombea anayekubalika
ndani ya Chama na nje ya chama ili kuirejesha Arusha ya kijani.
Miongoni mwa watia nia ambaye alikuwa anapigiwa upatu ni pamoja na
Philimon Mollel na wanachama kuwa anaweza kupita katika tanuru la
mchujo katika vikao vya juu kwenye Kamati kuu na Halmashauri kuu ya
taifa ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa ana mtaji wa wapiga kura.
Mwaka 2015 Mollel aliwania ubunge na kuangushwa na Godbles Lema
ambapo aliibuka mshindi kura 68,848,huku Mollel akipata kura
35,907,huku idadi ya wapiga kuwa wakiwa 104,353.
Ni wazi CCM ina kibarua kigumu kwa mgombea yeyote atakayepitishwa
kuweza kukomboa kura 32,941 ambazo zilimfanya Lema kuibuka kidedea
Desember 13 mwaka 2015.
Pamoja na tofauti hiyo Mollel anajivunia mtaji wa wapiga kura 35,907
waliompigia kura mwaka 2015 tofauti na wagombea wengine ambao hawana
mtaji wa wapiga kura.
Licha ya kura kutokutosha mwaka 2015 Mollel amekuwa karibu na chama
toka wakati huo akitoa misaada mbali mbali kwa wananchi walio na
uhitaji na kumfanya awe kipenzi cha wana CCM na wapiga kura wa jimbo
la Arusha Mjini.
Mgombea mwingine ambaye ameonyesha nia ya kuvaa viatu vya Lema ni
Thomas Munisi ambaye ni mfanya biashara ya madini na Mwenyekiti wa CCM
Kata ya Themi.
Moses Mwizarubi ni mmoja wa vijana wasomi ambaye anafanya kazi benki
kuu Tawi la Arusha ambaye ni kipenzi cha vijana wengi ndani ya CCM
Wakili msomi Alberth Msando ambaye aliwahi kuwa Diwani Mjini Moshi
kupitia Chadema na baadaye kutimkia CCM na Rais John Pombe Magufuri
kumteua kuwa mjumbe wa kamati ya kuhakiki mali za Chama ni mmoja kati
ya wanaopewa nafasi ya kupambana n Lema uchaguzi mkuu mwaka huu.
Wakili msomi Edmund Ngemela ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa
Wilaya ya Arusha Mjini ni hazina kubwa ya wasomi ndani ya CCM ambo
kama akipewa nafasi ya kugombea ubunge Arusha Mjini nina hakika Chama
hakitajilaumu.
Aliyewahi kuwa Meya Jiji la Arusha Gaudence Lyimo na ambaye alikuwa
Diwani wa Kata ya Orelian na baadaye Kata ya Kimandolu ni hazina kubwa
ya wana CCM kutokana na uzoefu wa kuwa Meya Jiji la Arusha,pia ni
mhandisi wa ujenzi wa barabara na majengo.
Mrisho Mashaka Gambo ambaye aliwahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha na
Rais Dkt John Pombe Magufuri kutengua uteuzi wake kutokana na
kutokuelewana na Mkuu wa Wilaya Gabriel Daqarro na Mkurugenzi wa Jiji
Dkt Maulid Madeni .
Lakini ushindi wake wa kupata kura za maoni 333, huku Philemon Mollel
akipata kura 68,Wakili Albeth Msando akipata kura 13,Mstahiki Meya wa
zamani Gaudence Lyimo akipata kura 12,Moses Mwizarubi akipata kura 6
na Karisti Lazalo ambaye alikihama chake cha Chadema na kujiunga CCM
akimbulia kura 2,umeibua maswali na mashaka mengi,huku wagombe wenzake
wakimtuhumu kwa madai mbali mbali.
Mustafa Panju ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya BushBack Tours &
Safaris mwenye asili ya kiasia ni miongoni mwa wagombe wasio na doa
ndani ya CCM na nje ya CCM.
Victor Mollel ambaye ni afisa mapato Halmashuri ya Moshi Vijijini na
mjumbe wa kamati ya siasa Arusha Mjini ni moja hazina na viongozi wa
CCM miaka ijayo ambaye kama vikao vya maamuzi vitaona anafaa anaweza
kupambana na Godbres Lema wa Chadema ambaye akipewa jukwaa la
kujieleza ana uwezo wa kubadili uamuzi wa wapiga kura.
Samsoni Mwigamba ambaye kwa sasa yuko Chuo kikuu Dodoma ambaye awali
iliibuliwa na Chadema na kuwa mwenyekiti kanda kaskazini na baadaye
kuasisi Chama Cha ACT Wazalendo na baadaye kuamua kurudi CCM anapigiwa
chapuo na wasomi kuweza kugombea ubunge Arusha Mjini.
Ole Comolo Mollel mstaafu wa Benki ya NBC na mtaalamu wa maswala ya
Saccos ambaye aliwaahidi wana CCM kuwa iwapo watamchagua kuwa mbunge
wa Arusha Mjini atahakikisha kila Kata ina anzisha Soccos ili akina
mama na Vijana waweze kupata mikopo ili kuinua kipato chao kwa kuwa
hawana sifa za kukopeshwa na Benki.
Ole Comolo ambaye ni mzaliwa wa kata ya Olasti Jijini hapa,aliwahi
kufanya kazi katika matawi ya Benki hiyo Arusha Mjini,Namanga na
baadaye Dar-es-Salaam na amestaafu mwaka jana
Pamoja na watia nia wote niliowataja wajue kuwa iwapo mmoja wao
atapitishwa na CCM kugombea ubunge ajue ana mzigo mzito kuweza
kukomboa kura 32,941,na nina hakika idadi ya wapiga kura itakuwa
imeongezeka baada ya marekebisho ya daftari la wapiga kura na tume ya
Taifa ya uchaguzi