Mwandishi Wetu
Kiungo mkabaji , Papy Kabamba Tshishimbi ni miongoni mwa wachezaji saba walioachwa Yanga SC baada ya mikataba yao kumalizika.
Kwa ujumla Yanga SC imeacha wachezaji 14 – wengine saba wakisitishiwa mikataba yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo viwango vyao kushuka, au kutokidhi mahitaji ya klabu.
Mbali na Tshishimbi, wengine walioachwa baada ya mikataba yao kumalizika ni Mkongo mwenzake, David Molinga ‘Falcao’ na wazawa Jaffary Mohamed, Tariq Seif, Andrew Vincent ‘Dante’, Mohamed Banka na Mrisho Ngassa.
Wanaoachwa kwa kusitishiwa mikataba yao ni Ally Mtoni ‘Sonso’, Muharami Issa ‘Marcelo’, Ali Ali, Muivory Coast Yikpe Gislain, Mnyarwanda Patrick Sibomana, Mzambia Erick Kabamba na Rapahael Daudi.
Baada ya kuachana na wachezaji hao 14, Yanga SC ipo kwenye mazungumzo na mabeki wake wakongwe wawili, Juma Abdul na Kelvin Yondan waliomaliza mikataba.
Wachezaji 15 tu kutoka kikosi cha msimu uliopita wamepitishwa kubaki ambao ni makipa Mkenya Farouk Shikhalo, Metacha Mnata na Ramadhan Kabwili na mabeki Paul Godfrey ‘Boxer’ na Mghana, Lamine Moro.
Wengine ni viungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Mghana Bernard Morrison, Feisal Salum, Juma Mahadhi, Adeyoum Ahmed, Said Juma ‘Makapu’, Balama Mapinduzi, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi na Abdulaziz Makame.
Tayari Yanga SC imesajili wachezaji wanne wapya, ambao ni mabeki Yassin Mustapha kutoka Polisi Tanzana ya Kilimanjaro, Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union ya Tanga, kiungo Zawadi Mauya kutoka Kagera Sugar na mshambuliaji Waziri Junior kutoka Mbao FC ya Mwanza iliyoshuka Daraja.