Mwandishi Wetu
KLABU ya Azam FC tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Ismail Aziz Kada, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Tanzania Prisons.
Kada amesaini mkataba huo leo Jumatatu mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, mara baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Kiungo huyo mshambuliaji, usajili wake ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.
Aidha, Kada amekuwa na msimu mzuri akiwa na Tanzania Prisons, akiwa amefunga jumla ya mabao matano na pasi tano za zilzozaa mabao.
Huo ni usajili wa nne kufanyika na timu hii kwenye dirisha hili kubwa la usajili, baada ya awali kusajiliwa Awesu Awesu, Ally Niyonzima na Ayoub Lyanga.