Afisa Lishe Mtafiti Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na lishe Tanzania, Bw. Walbert Mgeni akitoa ufafanuzi wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu mama kunyonyesha mtoto.
******************************
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Wazazi wametakiwa kutambua umuhimu kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama katika kipindi cha miezi sita hadi miaka miwili ili kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima ikiwemo saratani ya matiti.
Akizungumzia umuhimu wa wiki ya unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama Duniani, Afisa Lishe Mtafiti Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na lishe Tanzania, Bw. Walbert Mgeni, amesema kuwa kila mwaka kuanzia mwezi Agosti 1 hadi 7 Tanzania inaungana na nchi nyengine duniani kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji.
Bw. Mgeni amesema kuwa wazazi wanatakiwa kutambua maziwa ya mama ni muhimu hususani kwa watoto katika kipindi cha miezi sita, kwani maziwa hayo yanavirutubisho ambavyo vinazuia magonjwa mbalimbali kwa mtoto.
Amesema kuwa watoto wachanga wanapaswa kuanza kunyonyeshwa maziwa ya mama ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa ili maziwa yaanze kutoka mapema.
“Kumnyonyesha mtoto ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa kuna faida nyingi ikiwemo kusaidia maziwa ya mama kuanza kutoka mapema na mtoto kupata maziwa ya mwanzo ya njano” amesema Bw. Mgeni.
Mtaalam huyo ameeleza kuwa kuna maziwa ya njano ambayo ni maziwa ya mwanzo, mazito yenye rangi ya njano utoka siku chache za mwanzo baada ya kujifungua.
Amesema kuwa maziwa hayo ni chakula kamili chenye virutubisho vingi, na pia yanatoa kinga maalum dhidi ya maradhi.
Licha mtoto kupata virutubisho akitumia maziwa ya mama, lakini kuna faida nyingi kwa mama kunyonyesha ikiwemo msaidia kuepuka kupata magonjwa ya saratani ya matiti.
Amefafanua kuwa kuna changamoto zinazokabili khali ya lishe kuwa ni kuamini mila na destuli potofu watoto kuachishwa kunyonyeshwa mapema pamoja na uelewa mdogo kuhusu maswala unyonyeshaji.
Katika kukabiliana na changamoto hizo wanaendelea kutoa elimu ya unyonyeshaji na lishe ili kuhakikisha watanzania wanakuwa na afya bora