*******************************
Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Bwana Gerald Kusaya mapema leo tarehe 29 Julai, 2020 ametembelea Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu na baadae alielekea katika Viwanja vya Nyakabindi kwa ajili ya kujionea maandalizi ya mwisho ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) Kitaifa mkoani Simiyu.
Awali katika mazungumzo yake na Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Bwana Ekwabi Mujungu amemweleza Katibu Mkuu Kusaya kuwa maandalizi kwa upande wa mkoa wa Simiyu na Halmashauri zake yanaendelea vizuri na kuongeza kuwa huduma ya ujenzi wa mahema kwa Washiriki imekamilika kwa zaidi ya asilimi 90 na kuongeza kuwa huduma nyingine za kijamii kama umeme na maji zinaendelea kuimalishwa.
Baadae Katibu Mkuu Kusaya aliekea katika Viwanja vya Nyakabindi ili kujionea na kukagua maandalizi ya eneo la maonyesho ikiwa ni pamoja na kujionea jengo la Wizara ya Kilimo ambalo litakuwa sehemu ya kutolea mafunzo ya kudumu kwa Wakulima wa Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara na baadae alitembela maeneo yenye vipando vya mazao mambalimbali ambavyo vitatumia kwa ajili ya kufundishia teknolojiambalimbali za kilimo.
Baadae Katibu Mkuu Kusaya alitembelea mabanda ya Jeshi la Mageleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Katika mazungumzo yake na Wanahabari; Katibu Mkuu Kilimo Bwana Kusaya amesema; Wizara kwa kushirikiana na Wizara za Sekta ya Kilimo pamoja na Serikali ya mkoa wa Simiyu, Shinyanga na Mara imejipanga ili kuyafanya Maadhimisho ya Nane Nane 2020 kuendelea kuwa darasa la kutoa elimu kwa Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wanaushirika kutoka katika mikoa inayounda Kanda ya Magharibi ya Ziwa Victoria na mikoa jirani.
“Napenda kuwakaribisha Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na Wanaushirika wote wa mikoa hii pamoja na mikoa jirani kuja kushiriki, kujifunza na kujione maendeleo makubwa ya Sekta ya Kilimo na maandalizi kwa upande wetu Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Serikali ya mkoa wa Simiyu, Shinyanga na Mara yanaendelea vizuri, Tarehe 1 Agosti, 2020 tunataraji kuwa na Mgeni wetu Rasmi; Mama Samia Suluhu Hassan ambaye atafua rasmi Maadhimisho ya mwaka huu na baadae Rais wa Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli atahitimisha; Nawakaribisha Wananchi wote.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kilimo Bwana Gerald Musabila Kusaya.