***************
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars, Emmanuel Amunike,anamatumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa pili wa mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Kenya,katika mchezo utakaofanyika Juni 27,katika Uwanja wa 30 Juni,Misri.
Akizungumza na waandishi wa habari,Amunike,alisema anatambua Kenya ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri,lakini hilo halimpi shida kwakuwa viwango vya wachezaji wa Kenya na vya wachezaji wa Tanzania vinalingana,hivyo hana wasiwasi wa kupata matokea katika mchezo huo..
“Timu zote ni za kutoka Afrika Mashariki na Kenya ni majirani zetu,na wote tunazungumza lugha ya Kiswahili,kwahiyo hakuna kitu cha kujificha ,kitu kikubwa ni kwamba ni kwa jinsi gani tutaweza kufanya katika huo mchezo,tulionao katika mchezo wa Senegal wachezaji walikuwa na uoga,lakini siwezi kuwalaumu, kwakuwa haya ni mashindano yao makubwa kucheza,”alisema na kuongeza:
“Kitu kikubwa cha muhimu ambacho tunachokifanya kwasasa ni kuwapa moyo kuwajenga kiakili na kuwajengea ubora zaidi uwanjani wachezaji kabla ya mchezo wetu unaofuata,binafsi nina wachezaji bora na wenye uwezo,kwahiyo katika soka la kisasa naamini wanasifa za kushindana.”
Taifa Stars,inatarajia kushuka dimbani Alhamisi wiki hii, ikiwa na matumaini ya kupata alama tatu muhimu, ambazo zitaisaidia kuiweka katika mazingira mazuri ya kuweza kupata nafasi ya kufuzu kwa raundi ya pili ya mashindano.