Mheshimiwa Waziri wa Madini Dotto Biteko wakati akiongea kwenye tukio hili la utiaji sahihi mkataba kati ya STAMICO na GGM Mkurugezi wa GGM Bw.Richard Jordison naye akiweka sahihi kwenye mkataba wa Kandarasi ya uchorogaji miamba na STAMICO Wakuu wa mashirika haya mawili wakionesha mikataba baina yao baada ya kusainiwa. Kaimu Mkurugezi wa Stamico Dkt. Venance Mwasse akiweka sahihi kwenye Mkataba na GGMMwenyekiti wa Bodi ya Stamico, Mej Generali mst M.J Isamuhyo akiongea wakati wa tukio hili.Viongozi Wakuu wa STAMICO na GGM wakibadilishana mkataba mbele ya wanasheri wao na Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO. Mej. Generali mst M. J Isamuhyo na Richard Jordison Mkurugenzi wa GGM.
***********************************
Shirika la STAMICO limesaini mkataba wa kandarasi ya uchorogaji miamba na kampuni ya Madini ya GGM.
Makubaliano hayo yamefanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Geita na kuhudhuria na viongozi mbali mbali wa Serikali na kampuni ya GGM. Mgeni Rasmi kwenye tukio hilo alikuwa Mhe. Waziri wa Madini Doto Mashaka Biteko.
Tukio hilo lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Eng Robert Gabriel, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof Simon Msanjila, RAS mkoa wa Geita, Mkuu wa Wilaya na Viongozi na wafanyakazi kutoka STAMICO na GGM.
Katika hotuba yake Mheshimiwa Waziri amelipongeza sana Shirika la STAMICO kwa kazi nzuri wanayofanya
hasa katika kuwasaidia wachimaji wadogo wa madini na kuchangia pato la Taifa.
Kuhusu mkataba na GGM aliwaelekeza STAMICO kufanya kazi kwa bidii na Uaminifu wa kiwango Cha juu ili kujenga jina la STAMICO.
“Kandarasi Hii ni ya kwanza kwa hivyo tufanye kazi hii kwa viwango vya Juu kwa kutumia ujuzi wetu wote” amesema Biteko.
Ameongeza kuwa Kandarasi Hii ni Karata na tuicheze vizuri najuwa tutashida kwani STAMICO ina uongozi Bora na wafanyakazi waliosoma na wanaojuwa kufanya kazi hii” Kwa pande wa Mwenyekiti wa Bodi Mej Generali mstaafu M.J Isamuhyo alishukuru Wizara kwa kuiamini STAMICO na kumhakikishia Waziri kufanya kazi hii kwa weledi mkubwa na kutekeleza maagizo yote yaliyotuleta kwa STAMICO.
Kaimu Mkurugezi Mtendaji wa SMC Dkt. Venance Mwasse na Mkurugenzi Mtendaji wa GGM Bw. Richard Jordinson waliweza kutiliana sahihi na mbele ya Viongozi wengine wa kitaifa.