Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Tanzania Sabasaba Moshingi akiongea na wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari ya wasichana Feo iliyopo wilayani Songea wakati alipokwenda kukabidhi kompyuta 10 kwa ajili ya shule hiyo,katikati ni meneja wa shule Omari Msigwa,wa pili kushoto meneja wa TPB tawi la Songea Richard Chacha na wa kwanza kushoto Afisa mwandamizi kitengo cha mahusiano na mawasiliano wa Benki hiyo Chichi Banda.
Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Songea Richard Chacha akiongea na Jumuiya ya shule ya Sekonfdari ya wasichana Feo iliyopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,mara baada ya Benki hiyo kukabidhi kompyuta 10 kwa shule ya Feo
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Feo iliyopo katika kijiji cha Luhimba Halmashauri ya wilaya Madaba mkoani Ruvuma Moses Mbwilo akiongea jana kabla ya kupokea msaada wa Kompyuta 10 kutoka Benki ya TPB Tanzania,katikati Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi na wa pili kushoto Meneja wa Shule Omari Msigwa,
,Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Feo iliyopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,wakimsikiliza jana Mtendaji Mkuu wa Bebki ya TPB Tanzania Sabasaba Moshingi(hayupo pichani) aliyefika shuleni hapo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa kompyuta kwa shule hiyo.
Meneja wa shule ya sekondari ya wasichana Feo Omari Msigwa kulia, akipokea moja kati ya kompyuta 10 kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Tanzania Sabasaba Moshingi kushoto ili zisaidie wanafunzi kujifunzia na walimu kufundisha masomo kwa wanafunzi wa shule hiyo ambayo imetajwa ni miongoni mwa shule bora za wasichana zinazofanya vizuri kitaaluma mkoani Ruvuma
Na Mwandishi Wetu,Ruvuma
BENKI ya TPB Tanzania imetumia zaidi ya shilingi milioni 15 kununua kompyuta kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Feo(Feo Girls)iliyopo wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma ili kuwaongezea hamasa ya wanafunz na walimu wa shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma.
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Sabasaba Moshingi alisema, msaada huo ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii na ahadi aliyoitoa wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwaka uliopita.
Alisema, kwa kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na shule ya Sekondari ya Wasichana Feo Bebki ya TPB imeona ipo haja kubwa kuhakikisha inatoa sehemu ya faida yake katika kuchangia upatikanaji na utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Moshingi alisema, kompyuta hizo zinakwenda kuchochea hali ya kujisomea kwa wanafunzi wa shule hiyo pekee ya Wasichana inayofanya vizuri kitaaluma katika mkoa wa Ruvuma na walimu kutumia kwa ajili ya kuandaa masomo na mitihani kwa wanafunzi.
Alisema Benki ya TPB imeanzishwa miaka 95 iliyopita wakati Tanzania ikiwa katika utawala wa ukoloni na kati ya Benki zinazoendelea kufanya vizuri mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka 2019 pekee iliweza kutengeneza faida ya shilingi Bilioni 25 na tawi la Songea ndilo lililofanya vizuri kati ya matawi 74 hapa nchini kwa kutengeneza faida na kutoa huduma bora kwa wateja.
Alisema, mwaka 2019 Benki ya TPB inatenga kiasi cha fedha kila mwaka kwa ajili ya kusaidia huduma mbalimba,I za kijamii na mwaka jana TPB ilitenga shilingi milioni 300 kati ya hizo milioni 15 zimetumika kununua kompyuta 10 kwa ajili ya shule hiyo.
Amewataka watanzania wakiwemo wafanyakazi wa Feo Sekondari kutumia huduma bora za kibenki za TPB ili kunufaika na huduma zake ikiwemo mikopo zinazowalenga watu binafsi,wafanya biashara wadogo,wa kati na makampuni.
Alisema, Benki ya TPB inajivunia mchango mkubwa inaoutoa katika kusaidia huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali hapa nchini na kwa wafanya biashara,jambo lililoipaisha Benki hiyo kuwa moja kati ya Benki Bora na inayofanya vizuri hapa nchini.
Kwa mujibu wa Moshingi ni kwamba,katika kuonyesha inawathamini wateja na kutambua umuhimu wa mchango wao katika kuchangia huduma na uchumi kwa Taifa, TPB imekuwa mstari wa mbele kutoa mikopo ya aina mbalimbali kama fedha ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya kupunguza hali ya umaskini hapa nchini.
Moshingi ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo amempongeza Meneja na mmiliki wa shule shule hiyo Omari Msigwa kwa kujenga shule mzuri ambaye imekuwa ikiendelea kufanya vizuri kitaaluma kwa wanafunzi wake kupata alama za juu katika mitihani ya kiwilaya,mkoa na kitaifa.
Aidha, amewapongeza wanafunzi na walimu wa shule hiyo kutokana na matukio mazuri ya mitihani ya kidato cha pili na matokeo ya kidato cha nne mwaka uliopita ambapo shule ya Sekondari ya Wasichana Feo ilishika nafasi ya kwanza wilaya ya Songea na ya pili katika mkoa wa Ruvuma.
Amewatka kutumia msaada huo kuwaongezea maarifa na kujisomea zaidi ili waweze kufanya vizuri zaidi kitaaluma na kuwa na malengo ya kufanya vizuri katika masomo na mitihani yao na kuhakikisha wanashika nafasi ya kwanza kitaifa kitaaluma.
Alisema, ni lazima wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kuweka malengo maalum ambayo yatawawezesha hata watakapo maliza elimu ya juu waweze kumudu soko la ajira katika Nchi wanachama wa Jumuiya Afrika Mashariki na katika nchi mbalimbali Afrika na Dunia nzima kama ilivyo kwa watu wa mataifa mengine wanaokuja kufanya kazi hapa nchini Tanzania.
Meneja wa shule ya FEO Sekondari Omari Msigwa ameishukuru Benki ya TPB kwa msaada huo na kuhaidi kuwa kompyuta hizo zinakwenda kuhamasisha na kuchochea wanafunzi na walimu wa shule hiyo kuongeza taaluma.
Amewataka wanafunzi kuzitumia kompyuta kujifunza maarifa mbalimbali hasa ikizingatia kuwa Dunia kwa sasa ni kama kijiji kwa hiyo ni vizuri wanafunzi hao kutumia kompyuta hizo kusoma kwa bidi.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Luciana Msabila alisema, shule ya Sekondari ya Wasichana Feo ilianzishwa mwaka 2016 ikiwa na jumla ya wanafunzi 78 kwa mikondo miwili ya A na B pamoja na walimu 7,hata hivyo kwa sasa shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 300 na walimu 15.
Alisema, tangu ilipoanzishwa shule imefanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili kwa miaka mitatu mfululizo 2017,2018 na 2019.
Alisema, katika matokeo ya mwaka jana ambayo ni ya kwanza kwa wanafunzi wa kidato cha nne tangu ilipoanzishwa, kati ya wanafunzi 62 waliofanya mtihani huo waliopata daraja la 1 walikuwa (38)Daraja la 2 (22)daraja 3(2) na hakuna aliyepata daraja la nne wala aliyefeli.
Alisema, shule hiyo ilifanikiwa kushika nafasi ya 1 Kiwilaya,nafasi ya pili Kimkoa na Kitaifa ilishika nafasi ya 63 ambapo imeweka mikakati ya kufanya maboresho ili waweze kufanya vizuri zaidi kitaaluma na kinidhamu.