Mwandishi na Mtangazaji nguli na wa siku nyingi hapa nchini Angel Akilimali amejitosa kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuteuliwa kuwa mgombea wa Ubunge jimbo la Ukonga kwa tiketi ya CCM, katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Pichani, Angel ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM akionyesha fomu yake baada ya kuichukua leo, katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala, leo.