Mwanachama Wakili Ericky Kidyalla (Kulia)akikabidhiwa fomu yakugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kibamba Jijini Dar es Salaam.
Mwanachama Wakili Ericky Kidyalla akionesha fomu alizochukua kwaajili ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kibamba.Mwanachama Wakili Ericky Kidyalla (Kushoto) akipata picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa CCM waliofika katika Ofisi ya Chama hicho kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge.
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Mwanachama ambaye pia ni mjumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wakili Ericky Kidyalla amechukua fomu ya kugombea Ubunge kwenye jimbo la Kibamba Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu amesema anahitaji kuwaonesha na kuwa mfano kwa vijana wanachama ambao hawana vyeo vyovyote kuwa wanaweza kuchukua fomu na kugombea nafasi ya uongozi ili kuweza kuwatumika wananchi.
“Huu msimu ambao tunahitaji kuingia vijana wenye weledi, vijana tuliosoma na tunajua jamii yetu inatakiwa kuelekea wapi hivyo tunahitaji kuendeleza kasi ambayo ameianzisha Mweneyekiti wetu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli”. Amesema Wakili Kidyalla.