Bilionea mpya nchini Tanzania ambae ni Mchimbaji wa Madini Bw. Saniniu Laizer, akisaini daftari la wageni wakati alipofika kutembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa Tehama kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Maendaenda akimuonesha Bw. Saniniu Lazier, mfumo wa kielektroniki unaoonesha muenendo wa makusanyo ya Serikali kwa Taasisi zote za kwa kila siku ikiwa ni njia ya kuongeza uwazi na kudhibiti makusanyo ya fedha za umma, wakati alipotembelea banda la Wizara pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa Tehama kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Maendaenda akimuonesha Bw. Saniniu Lazier, namna ya kufanya Malipo ya Huduma za mbalimbali kwa kutumia (GEPG- App) ambayo inawawezesha watumiaji kuhakiki namba ya malipo (Control Number), kutathmini na kulipa malipo ya Serikali kupitia huduma ya simu za mkononi, wakati alipotembelea banda la Wizara pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa Tehama kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Maendaenda akimueleza Bw. Saniniu Laizer, namna Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Huduma za Serikali ambavyo umeweza kupunguza gharama za ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kuondoa ada ya miamala kwa Taasisi za umma na kuwezesha taarifa sahihi za mapato ya Serikali kupatikana kwa wakati, wakati alipotembelea banda la wizara pamoja na taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano kwa Umma (PSPTB) Bi. Shamim Mdee, akimueleza Bw Saniniu Laizer, kuhusu majukumu mbalimbali ya Bodi ya PSPTB ikiwemo kusajili watoa huduma za ununuzi na ugavi, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Ramadhani Kissimba (kushoto) akimuongoza Bw. Saniniu Laizer, kutembelea banda la Wizara pamoja na Taasisi zake wakati alipotembelea banda hilo kujionea huduma na elimu inayotolewa kwa umma wakati wa Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango).