Mkurugenzi wa Mafunzo ,utafiti na takwimu ndugu Joshua Matiko akiongea kwenye semina hiyo liyofanyika jijini Dodoma
Washiriki wa semina wakifuatilia kwa makini juu ya mawasilisho toka kwa watoa mada mbalimbali toka OSHA Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mhandisi Alex Ngata akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya usalama na afya toka kwa washiriki wa semina waliyotaka kufahamu zaidi
Washiriki wa semina ya pamoja baina ya OSHA na wawakilishi wa waajiri kutoka maeneo mbalimbali ya kazi jiji la Dodoma wakisikilza mada zilizokuwa zinawasilishwa kwenye semina hyo jijini Dodoma.
*************************************
Mwandishi wetu, Dodoma
Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mhandishi Alex Ngata amewataka wadau kuendelea kutoa ushiriikiano kwa OSHA ili kuendelea kuboresha hali za wafanyakazi Maeneo ya kazi, kwa kuhakikisha kuwa usalama na afya sehemu za kazi zinazingatiwa.
Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, kwenye mafunzo ya vision zero mkoani Dodoma yaliondaliwa na OSHA, Ngata amesema OSHA imeendelea kuboresha huduma zake kwa wadau hao, hivyo hawanabudi kuhakikisha wanashirikiana naa OSHA wakati wote kwa kuhakikisha kaguzi zote za kisheria zinafanyika ili kukidhi matakwa ya sheria. Amesema OSHA imeboresha huduma zake kwa kuondoa tozo ambazo ni ada ya usajili sehemu za kazi, leseni ya kukidhi matakwa ya sheria, tozo ya vifaa vya kuzima moto,,fomu ya usajili amabazo zilikuwa kikwazo kwa waajiri kwa kuziondoa na zingine na hivi karibuni tumepunguza tozo ya uchunguzi wa ajali sehemu ya kazi ili kuwezesha waajiri kukidhi matakwa ya sheria.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa mafunzo , utafiti na Takwimu Ndugu Joshua Matiko amesema ili kuweza kufikia malengo hayo,, waajiri nchini wanatakiwa kuweka mifumo madhubuti ya Kulinda wafanyakazi wakiwa kazini, ikiwemo kuweka malengo kwenye mipango mikakati yao wanayopanga. Amesema menejiment ndio wenye jukumu la kusimamia masuala ya usalama sehemu za kazi kwani wasipoweka juhudi basi nivigumu kufanikiwa
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za tathimin toka mfuko wa fidia (WCF) Dr. Abdulasum Omary amesema watu takribani milioni 2 .3 wanapoteza maisha sehemu za kazi kila mwaka kutokana na ajali na magojwa yanayotokana na kazi
Kwa upande wao washiriki wa semina hiyo wamesema wameshukuru uongozi wa OSHA kwa kuona umuhimu wa kuendesha semina hiyo kwaajiri aitasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi. Na wamesema semina za mara kwa mara ziawasaidia kupata mambo mengi ambayo walikuwa hawayafamu.