Manchester United jana imeichapa Aston Villa 3-0 Uwanja wa Villa Park katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, mabao ya Bruno Fernandes dakika ya 27 kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Ezri Konsa, Mason Greenwood dakika ya 45 na Paul Pogba dakika ya 58. Kwa ushindi huo Manchester United inafikisha pointi 58, ingawa inabaki nafasi ya tano, ikizidiwa pointi moja na Leicester City baada ya wote kucheza mechi 34 PICHA ZAIDI SOMA HAPA