Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa Nkulabi,Kata ya Mpunguzi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari Nkulabi ili kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kufuata masomo moja ya ahadi yake.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akichimba msingi wa kuanza ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nkulabi ikiwa ni ahadi yake ya kuwajengea shule hiyo ili kuwasaidia wanafunzi.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akiwa na wananchi wa Nkulabi,Kata ya Mpunguzi wakiwa wamebeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nkulabi ikiwa ni ahadi yake ya kuwajengea shule hiyo ili kuwasaidia wanafunzi.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akisisitiza jambo kwa wananchi wa Nkulabi,Kata ya Mpunguzi wakati wa kuanza ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nkulabi ikiwa ni ahadi yake ya kuwajengea shule hiyo ili kuwasaidia wanafunzi.
……………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde leo ameongoza wananchi wa Nkulabi,Kata ya Mpunguzi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari Nkulabi ili kuwaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kufuata masomo.
Ujenzi huo umetokana na ombi la wananchi kwa mbunge huyo kutokana na kukosekana kwa Shule ya Sekondari iliyokaribu na maeneo yao, na hivyo Mavunde kukubali ombi lao na kuanza utekelezaji.
Akizungumza na wananchi wakati wa kuchimba msingi wa kuanza ujenzi wa shule hiyo ,Mavunde amesema ujenzi huo ni moja ya ahadi alizowahi kuzitoa huku akiwataka wananchi kuunga mkono Serikali na viongozi wao wenye nia ya kuwapelekea maendeleo
“Nawashukuru wananchi wote mliojitokeza hapa siku ya leo kwa kujitolea kwenu nguvu kazi na matofali zaidi ya 10,000 kufanikisha kuanza kwa ujenzi wa shule ya Sekondari Nkulabi, lazima wananchi tuungane na serikali pamoja na viongozi wetu kujiletea maendeleo yetu wenyewe,ninyi mmekuwa mfano wa wananchi wawajibikaji na ndio maana nimeamua kuwaunga mkono ili malengo yetu yatimie”amesema.
Ameahidi kugharamia gharama za mafundi zote za kujenga madarasa matatu,na pia kutoa mifuko 100 ya saruji ili kukamilisha ujenzi huo wa awali.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wa Nkulabi,Mzee Hudson Mathias Mhepwa amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kujitoa kwake kwa wananchi katika kushirikiana kwenye ujenzi wa Sekondari hiyo na kuahidi kuwa nae bega kwa bega mpaka kukamilika kwa ujenzi huo kwa kutoa mchango wa hali na mali.
Amesema ujenzi huo utasaidia watoto kusoma kwa bidii na kufaulu masomo yao.