Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri Tanzania, Bi.Pendo Berege, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa wanawake TALGWU Taifa kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya wafanyakazi Wanawake TALGWU Taifa Bi.Beatrice Njawa,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa wanawake TALGWU Taifa kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia ufunguzi wa mkutano wa chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa wanawake TALGWU Taifa kilichofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na Majid Abdulkarim Dodoma.
Katika kuhakikisha tatizo la ukatili wa kijinsia kwa Wanawake mahala pa kazi linakomeshwa hapa nchini Wanawake wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi za juu za maamuzi katika vyama vya wafanyakazi.
Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri Tanzania, Pendo Berege, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa wanawake TALGWU taifa.
Amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia hususa ni vitendo unyanyasaji wa kingono kwenye maeneo ya kazi bado upo ili kukomesha vitendo hivyo ni wanatakiwa kuwa wengi katika ngazi za maamuzi.
“Wanawake mjitokeze kwa wingi kwenye ngazi za maamuzi vitendo hivi vitakomeshwa, Wanawake kwenye uongozi ni wachache Sana, kwenye Wizara tunavyama thelathini na nne(34) lakini ukiangalia Wanawake ni wachache Sana” amesema bi Pendo.
Aidha amewataka Wanawake kuwa waaminifu katika kutekeleza majukumu yao na kuendelea kufichua pale wanapoona wametendewa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
” Sio Sasa mnafanya Makosa kwa makusudi na mkigombezwa na waajiri wenu ndio Sasa mnasingizia kufanyiwa ukatili wa kijinsia hiyo sio sawa kabisa” amesema.
Pia amewataka viongozi waliohudhuria mkutano huo kutoka mikoa yote ya Tanzania bara kwenda kuyafangia kazi yale yote waliojifunza kupitia mkutano huo na kwenda kuwashirikisha wafanyakazi wengine ambao hawakufika katika mkutano huo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya wafanyakazi wanawake TALGWU taifa bi Beatrice Njawa, amesema mkutano huo ni wa siku mbili wenye lengo la kujadili namna bora ya utekelezaji wa majukumu yao.
Na wameahidi kwenda kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma iliyobora kwa wananchi wanaowahudumia katika maeneo yao.
Ameongeza kuwa”tunaomba serikali ikemee vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwani vimekuwa vikiwaondolea utu Wanawake katika maeneo yao ya kazi” amesema bi. Njawa.
Aidha ameitaka serikali kuboresha miondombinu kuwa inayompa staha mwanamke pindi anapokuwa katika eneo lake la kazi kama vyoo na sehemu za kujisitili.