Afisa Msadizi wa Benki, Bw. Robert Bukori kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki BoT, akitoa elimu kuhusu historia ya noti zetu kwa wananchi waliotembelea Banda la BoT Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi wa Benki, Bw. Gideon Rwegoshora kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha BoT, akitoa elimu kuhusu usimamizi wa sekta hio kwa mwananchi alietembelea Banda la BoT Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa Benki, Bi. Restituta Minja, kutoka kurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT akitoa elimu kuhusu namna ya kutambua alama za usalama katika noti zetu kwa wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT, walipotembelea Banda la BoT Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Rasimali Watu, Bi. Joyce Shala, kutoka Bodi ya Bima ya Amana akitoa elimu kuhusu Bodi hio kwa wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT, walipotembelea Banda la BoT Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Mipango, Bw. Shamy Chamicha, kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, akitoa elimu kuhusu uchumi wetu kwa wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT, walipotembelea Banda la BoT Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Sheria, Bw, Aclay Chaula, kutoka Bodi ya Bima ya Amana (DIB) akitoa elimu kuhusu Bodi hio kwa wananchi waliotembelea Banda la BoT Sabasaba jijini Dar es Salaam.