……………………………………………………………
KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE] BILA KIBALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia PASCHAL MAYEGE [38] Mkazi wa Mkola Wilayani Chunya kwa tuhuma za kumiliki silaha bunduki aina ya Gobole bila kuwa na kibali.
Mtuhumiwa alikamatwa katika msako uliofanyika tarehe 30.07.2020 majira ya saa 19:00 Jioni huko katika Kitongoji na Kata ya Mkola, Tarafa ya Kipembawe,Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa alikamatwa na silaha hiyo isiyokuwa na namba za usajili ndani ya nyumba anayoishi. Upelelezi unaendelea.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA UVUNJAJI NA UPORAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa thelathini na moja [31] wote wanaume kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvunjaji, uporaji na vitendo vingine vya uhalifu katika maeneo mbalimbali Jijini Mbeya.
Watuhumiwa wamekamatwa katika misako iliyoendeshwa na Jeshi la Polisi katika maeneo ya Nanenane, Uyole, Uyole Kati, Itezi na Nyigamba katika vilabu vya pombe za kienyeji wakinywa pombe huku wengine wakicheza kamali.
Aidha katika misako hiyo, zimekamatwa Pikipiki tatu [03] zinazodhaniwa kuwa ni mali za wizi ambazo ni:-
- MC.413 AQQ aina ya San lg.
- T.143 BTH aina ya Fekon.
- Pikipiki aina ya T-Better isiyo kuwa nan amba ya usajili.
Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA MAUAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne 1. MPESSO NJAGAJA @ MOPOZE [40], 2. MBALAMWEZI SASAJILA [42], 3. MAATON HAUS [51] na 4. LAMECK HAUS [60] wote wakazi wa Ikukwa kwa tuhuma za mauaji ya ELIAS NZIYAJE @ MIYOMBE [41] tingo wa lori la Mapembelo.
Watuhumiwa wamekamatwa mnamo tarehe 02.07.2020 majira ya saa 02:00 usiku huko Kijiji na Kata ya Ikukwa, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya baada ya kutafutwa kwa muda mrefu kutokana na tuhuma za kuhusika katika tukio la mauaji ya ELIAS NZIYAJE @ MIYOMBE [41] lililotokea mnamo tarehe 24/05/2020 huko Kijiji na Kata ya Ikukwa, Wilaya ya Mbeya Vijijini. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
MAUAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia UPENDO ANYIMIKE MWANG’ONDA [48] Mkazi wa Ilima kwa tuhuma za mauaji ya SINARAHA MWANG’ONDA [84] Mkazi wa Ilima.
Tukio hili limetokea tarehe 02.07.2020 majira ya saa 18:00 jioni huko Kijiji na Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya ambapo SINARAHA MWANG’ONDA [84] mkazi wa Ilima aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani akiwa amelala nyumbani kwake.
Chanzo cha tukio hili ni tuhuma za wizi kwani tarehe 01.07.2020 majira ya saa 13:00 Mchana marehemu alituhumiwa kuiba Pipa mali ya UPENDO ANYIMIKE MWANG’ONDA alishitakiwa kwa Balozi na aliamriwa alipe fedha taslimu kiasi cha Tshs.20,000/= kama fidia lakini hakuonekana mpaka alipokutwa ameuawa.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa uchunguzi wa kitabibu. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.
AJALI YA MOTO NA KUSABABISHA KIFO.
Mnamo tarehe 02.07.2020 majira ya saa 16:30 Jioni huko Kitongoji cha Jejere, Kijiji cha Mahongole, Kata ya Imalilo Songwe, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya. Mtoto MASELE JOSEPH, miezi 04 na mkazi wa Mahongole alifariki dunia baada ya kuungua moto akiwa amelazwa na mzazi wake katika kibanda cha nyasi shambani.
Chanzo cha tukio ni uzembe wa mzazi kutokuwa makini kwa mtoto wake PENDO JOSEPH miaka 04 aliyechoma kibanda hicho kwa kibiriti wakati mzazi wake akiwa shambani. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Mbarali. Upelelezi unaendelea.
KUPATIKANA NA BHANGI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia MBESO NJANGAJE @ MWAMPOZIA [40] Mkazi wa Ikukwa katika Halmashauri ya Mji Mdogo Mbalizi akiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi yenye uzito wa kilo 10 na gramu 215.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 02.07.2020 majira ya saa 02:00 Usiku huko Kitongoji cha Itende – Juu, Kijiji na Kata ya Ikukwa, Tarafa ya Usongwe. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi na atafikishwa mahakamani leo tarehe 03.07.2020.