********************************
Na Magreth Mbinga
Mratibu msidizi wa Jeshi la zimamoto Mkoa wa Kipolisi Ilala Inspekta Elisa Mugisha amewahimiza wafanyabishara ambao wanauza vifaa vya kuzimamoto wawe na kibali Cha kuweza kufanya biashara hiyo.
Amezungumza hayo leo Makao Makuu ya Jeshi la zimamoto na uokoaji na kuwataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi moto unapotokea kuweza kufika eneo la tukio mapema.
Pia Inspekta Mugisha amesema mpango kazi wao ni kutoa elimu kwa umma dhidi ya majanga mbalimbali yanayotokea katika jamii pamoja na kuzima moto na kuokoa maisha na mali.
“Elimu kwa umma imetolewa kupitia mikutano ya Serikali za mitaa,mashuleni,mamasokoni na miadhara”amesema Mugisha.
Vilevile amesema wamefanikiwa kutoa elimu kwenye televisheni na Redio kwa jumla ya vipindi 122 hivyo elimu ya kinga na tahadhari ya Moto imeendelea kutolewa kwenye sehemu mbalimbali za mikusanyiko kwa jumla ya maeneo 100 ya Mkoa wa Ilala.
Sanjari na hayo Inspekta Mugisha amesema kwasasa matukio ya Moto yamepungua kulinganisha na miaka iliyopita 2017-2018 matukio 184, 2018-2019 matukio 160 na mwaka 2019-2020 matukio 139.
“Hii inatokana kwamba tumefanikiwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma kuhusu kujikinga na majanga dhidi ya moto”amesema Mgisha.
Hata hivyo Mugisha amesema Mkoa wao kwa mwaka huu wamepokea misaada mbalimbali mfano katika chumba cha vifaa vya upumuaji wamepokea misaada kutoka kwa wadhamini .
“Back plate aina ya PSS 5000-50,Back plate aina ya Drager – 122,Back plate ambazo hazijatimia aina ya Drager -25, Tester ya face mask-02, Euro tester-01, Filter za compresor -05, BA Cylinder Aina ya Carbon-16, LDV-200, Pneumatic system-10, Face mask-07 na Compressor-01” amesema Inspekta Mugisha.