Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli (mwenye shati la kijani), akishirikiana na wasimamizi wa mradi ya ukarabati wa maegesho ya magari kwenye ofisi za CCM mkoa jana.
Picha na Baltazar Mashaka
********************************
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli wakati akihojiwa na Uhuru kuhusu uboreshaji huo wa ofisi miradi mingine ya maendeleo.
Alisema uboreshaji wa ofisi ya CCM Mkoa wa Mwanza unaofanywa chini unazidi kupamba moto na kufanya madhari yake kuvutia na kuirejesha katika ubora wake.
Alisema wamefanya maboresho ya kupaka rangi jengo lote la ofisi hiyo ya CCM mkoa (ndani na nje) pamoja na kuliwekea malumalu (vigae) kwenye sakafu baada ya miaka mingi kupita na hivyo kufanya madhari yake yavutie.
“Kamati ya Siasa ya Mkoa chini ya Mwenyekiti Dk. Anthony Diallo uliamua kufanya maboresho ya Uwanja wa CCM Kirumba uliotumika kwa maadhimisho ya Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri, tuliboresha Jukwaa Kuu na kujenga majukwaa mengine madogo mawili kwenye uwanja huo,”
“Maboresho mengine yaliyofanyika ni ukarabati mkubwa wa jengo la ofisi yaa CCM Mkoa ambao ulikuwa ni kulipaka rangi ndani na nje pamoja na kuliwekea vigae kwenye sakafu.Yote hayo yamefanyika kwa ajili ya maendeleo na kusababisha vikao vya maandalizi ya ilani vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama vilifanyika hapo,”alisema Kalli.
Alisema kazi kubwa iliongezeka ni ya ukarabati wa eneo la maegesho ya magari ambalo liliharibika ambapo kazi inayofanyika ni kuliwekea tyries baada ya kukamilika litatumika kiuchumi