***************************
MJUMBE wa kamati Kuu ya CCM , Mhe Balozi Seif Ali Idd amewataka wanachama wa chama hicho waliotia nia ya kugombea nafasi za Udiwani, Uwakilishi na Ubunge kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Balozi Seif ametoa kauli wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Micheweni.
Amesema Chama hakitasita kufuta jina la mwanachama ambaye atabainika kutumia fedha kushawishi ili jina lake lipitishwe.
amesema wanchama wanapaswa kuwatolea taarifa mamlaka husika wagombea ambao wanatumia fedha kununua uongozi ili wachukuliwe hatua.
Aidha amewataka kuendelea kudumisha umoja wakati wa mchakato wa kumpata mwanachama atakayepeperusha bendera ya CCM kuwania Urais wa Zanzibar huku akiahidi kupatikana mwanachama ambaye ni muumini wa Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12,1964.