Lionel Messi akishangilia baada ya kufunga Barcelona bao la pili kwa penalti dakika ya 50 katika sare ya 2-2 na Atletico Madrid kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou, hilo likiwa bao lake la 700 tangu aanze soka na la 630 katika klabu hiyo. Bao la kwanza Diego Costa alijifunga dakika ya 11, wakati mabao ya Atletico Madrid yalifungwa na Saul kwa penalt yote dakika ya 19 na 62.
Cristiano Ronaldo ni mchezaji mwingine pekee wa sasa zaidi ya Messi aliyefunga mabao 725 katika mechi 1002 akiwa na klabu za Sporting, Manchester United, Real Madrid, Juventus na timu yake ya taifa ya Ureno.
Josef Bican anaendelea kushikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote kwenye mechi za mashindano kwa mabao yake 805 aliyofunga akiwa na Rapid Vienna, Slavia Prague zote za Austria na timu za taifa za Czechoslovak.
Wanaomfuatia Bican ni Romario mabao 772, mechi 994, Pele mabao 767, mechi 831, Ferenc Puskas mabao 746, mechi 754, Gerd Muller mabao 735, mechi 793 na Mbrazil, Ronaldo mabao 725, mechi 1002.
Na Sare hiyo inaifanya Barcelona ibaki nafasi ya pili ikifikisha pointi 70 baada ya kucheza mechi 33, ikiziwa pointi moja na vinara, Real Madrid ambao pia wana mechi moja mkononi, wakati Atletico Madrid inabaki nafasi ya tatu pia sasa ikifikisha pointi 59 baada ya kucheza mechi 33 pia PICHA ZAIDI SOMA HAPA