*******************************
Na Magreth Mbinga
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda ampatia siku 30 Mkandarasi anaejenga jengo la Manispaa ya Ubungo kukamilisha ujenzi huo .
Hayo yametokea Leo wakati wa kukabidhi miradi iliyojengwa katika Wilaya hiyo katika Jimbo la Kibamba.
RC Makonda amesema mradi huo ulitakiwa ukamilike December 2019 lakini haukukamilika na akaomba muda wa miezi 6 na haujakamilika mpaka sasa.
Vilevile Rc Makonda amekabidhi miradi iliyotekelezeka katika kata ya Kibamba ambayo ni Daraja la juu lililopo Kibamba CCM,Tanki la maji la Lita milioni10 ambalo linapeleka maji Kisalawe .
Sanjari na hayo RC Makonda amesema Kuna miradi mingine ambayo itaanza kutekelezwa Kama ujenzi wa barabara za mitaa zenye jumla ya km 111 na Tanki la maji litakalojengwa Mbezi Msakuzi litakalo sambaza maji maeneo ya Msakuzi,Mpiji Magoe .
Hatahivyo amekabidhi stand ya mabasi ya kipekee Africa Mashariki na kati yaendayo mikoani na nje ya nchi ambayo itakuwa na maeneo ya biashara,parking za magari makubwa na madogo na inathamani ya Bilioni 50 na Milioni 900 na Sasa umefikia 72%.
“Ndani ya stendi kutakuwa maeneo ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga, bodaboda , mama lishe ,kumbi za sinema , maduka makubwa(super market) na hoteli kwaajili ya wasafiri”amesema RC Makonda.
RC Makonda amekabidhi zahanati ya Saranga kwa Chama Cha mapinduzi kwaajili ya kuimarisha huduma ya afya katika Wilaya hiyo ya Ubungo hasa Jimbo la Kibamba.
Mkuu wa Wilaya hiyo ya Ubungo Dc Lucas Mgonja amesema ujenzi wa Daraja la Kibamba ulianza July 2018 na walipewa miezi 30 hadi Mei mwishoni mwaka huu umefikia 65% pia inatanua barabara ,madaraja makubwa 8 na madaraja 6 kwaajili ya mito .