……………………………………………………………….
Na.Alex Sonna, Dodoma
Waumini wa Dini ya Kislamu nchini wametakiwa kulinda na kudumisha amani na utulivu ulipo nchini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Mustafa Rajabu katika uchaguzi Mkuu wa Baraza la Wislam Ngazi ya Mkoa wa Dodoma.
Aidha Sheik Rajabu amesema kuwa waumini wa dini ya kislamu wanatakiwa kushirikian na serikali yao kw akaribu san ili kulinda amani na utulivu wan chini.
“Katika Uchaguzi tuhakikishe tunachangua viongozi bora watakao tusikiliza, kutuhudumia na kutatua shida za watanzania hivyo ni wakati sasa wa kujitathimi katika maeneo yetu.
Katika uchaguzi Mkuu wa Baraza la Wislam Ngazi ya Mkoa wa Dodoma Sheikh Rajabu ametoa wito kwa viongozi waliyo patikana mambao ni Mwenyekiti wa Mkoa BAKWATA, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa BAKWATA na Wajumbe wa Baraza la Bakwata Mkoa kuwa wajitambue katika nafasi zao ,wabadilike na kuhacha mazoea ndo daraja la kuleta maendeleo katika nafasi hizo.
“Iwapo yote hayo yatatekelezwa katika nyazifa zenu basi itakuwa kasi raisi sana kufanyikisha utendaji wenu katika ubora unaohitajika na jamii mnayoiongoza”, amesisitiza Sheikh Rajabu.
Naye Mwenyekiti Mpya wa Baraza la BAKWATA mkoa wa Dodoma, Sheikh Jaafari Mwanyemba ameshukuru kwa wajumbe waliyompatia ridhaa ya kuongoza katika nafasi hiyo huku akiomba kupatiwa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake ambayo ameweka kipaumbele cha kuanza na kuzitambua mali za BAKWATA na kutaka kuongeza mapato kupitia vitenga uchumi vya BAKWATA vilivyopo hapa mkoani.
Kwa Upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu BAKWATA, Sheikh Kakongwe Songoro amesema kuwa kila kiongozi katika nafasi yake aheshimu nafasi ya mwenzake ili Baraza na Mkoa kwa Ujumla kuweza kupata mafanikio yanayotarajiwa na waumini wanao waoongoza.
Lakini pia ametaka kuwe na uwazi katika utendaji wa uongozi mpya ili kutokuwa na migogoro, majungu na chuki baina ya viongozi wao kwa kwao na waumini wao.
Naye katibu wa Baraza la Wanawake BAKWATA Mkoa wa Dodoma Ukhut Jasmine akitoa wito kwa viongozi hao wapya waliyochaguliwa kuwa na ushirikiano na kumtanguliza Allah kwani kiongozi bora ni kioo cha jamii yake anayoiongoza.