***********************
Kocha Mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars,amesema wana imani kubwa ya kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo wa ufunguzi wa i dhidi ya Senegal,ambao ni mchezo wa kwanza utakaofanyika,Juni 21 katika Uwanja wa 30 June,Cairo,Misri.
Amunike amesema mpaka sasa wameweza kujiandaa kimbinu na kiakili katika mchezo huo ambao anatambua wanacheza na timu kubwa Barani Afrika, lakini hawana wasiwasi kutokana na maandalizi waliyoyafanya.
“Kikubwa katika mchezo huo,tumejiandaa kisaikolojia na kimbinu ili tuweze kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na tunaamini kesho utakuwa mchezo mzuri wa mashindano,na naamini wachezaji wangu wapo kamili kuweza kucheza mchezo huo na wanajua umuhimu wa mchezo huo.
Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars,Mbwana Samatta,alisema Kwamba wanawaheshimu Senegal kwakuwa ni timu kubwa Afrika ,lakini hawatokwenda uwanjani kinyonge.
“Kikubwa ni kwamba tutakwenda uwanjani,huku tukijua tunaenda kupambana na timu kubwa na lazima tupambane uwanjani ili tuwezee kulisogeze jina la nchi yetu,hivyo tunaamini kabla ya filimbi ya mwisho kila timu ina nafasi.”