Mhe.Bernadeta Kasabago Mushashu mbunge viti maalumu CCM Mkoa wa Kagera akiongea na viongozi wa wanawake wa jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania UWT kutoka kata zote za manispaa ya Bukoba akieleza mambo aliyoyafanya kwa kipindi cha miaka 5.
Mhe.Bernadeta Kasabago Mushashu mbunge viti maalumu CCM Mkoa wa Kagera wa kwanza kulia akimkabidhi Katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Kagera Comred Hamimu Mahamudu wapili kushoto kitita cha shilingi milioni mbili aliyoiahidi wakati wa uzinduzi wa Kagera ya Kijani kwaajili wa ukarabati wa ofisi ya CCM Mkoa.
Katibu mwenezi wa Mkoa wa Kagera Comred Hamimu Mahamudu akiwahutubia wakina mama wa manispaa ya Bukoba waliowawakilisha wakina mama wengine wa CCM.
Baadhi ya viongozi wa jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania UWT Kutoka kata zote za manispaa ya Bukoba wakimshangilia mbunge wao Mhe.Bernadeta Kasabago Mushashu alipokuwa akiwahutubia.
Picha zote na Allawi Kaboyo.
……………………………………………………………………………
Na Allawi Kaboyo,Bukoba
Kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba Mwaka huu vyama vya siasa na wanansiasa wamekuwa wakitangaza nia za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo kata,majimbo pamoja na nafasi ya Uarais wa Tanzania.
Akiongea mjini Bukoba juni 23,mwaka huu na viongozi wa umoja wa wanawake wa CCM (UWT) kutoka kata zote za Manispaa ya Bukoba Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Kagera Mhe.Bernadeta Mushashu amesema kumekuwepo na tabia ya watangaza nia kutoka katika chama hicho wanaowachafua madiwani pamoja na wabunge wanaomaliza muda wao wakitaka kuchukua nafasi zao.
Mhe.Mushashu ameleza kuwa amekuwa akipokea tuhuma nyingi kutoka kwa madiwani wa mkoa huo kuwa wanachafuliwa kwa kashifa nzito kutoka kwa wanachama wanaotaka kutangaza nia akiwemo yeye ambapo amewatahadharisha wale wote wenye tabia hiyo waache mara moja kwa kuwa chama chake bado kinawatambua kama viongozi.
“Nimesikitishwa na wanaccm wenzetu wanaotangaza nia za kugombea nafasi mbalimbali hapa mkoani mwetu kuanza kutuchafua na kututolea maneno ya kashifa kwa wananchi kisa uongozi hili sio jambo la kiungwana ndugu zangu, mimi mwenyewe nimeshasemwa mengi likiwemo hili la mimi kuwa mremavu wapo wanaosema kuwa sistahili kuwa mbunge kisa mimi ni mremavu wa miguu kuwa nikagombee viti maalumu vya walemavu kiukweli suala hili limeniuma sana.” Alieleza Mbunge Mushashu
Ameongeza kuwa wanaotaka nafasi za uongozi wala hawazuiliwi lakini wasiwachafue viongozi wanaomaliza muda wao kwa kuwasema vibaya na kuwapa tuhuma ambazo sio zao huku akifafanua kuwa wabunge na madiwani bado wananendelea na majukumu yao hadi hapo tarehe za kuchukua form za kugombea zitakapo timia na watauacha ubunge na udiwani pindi wabunge na madiwani wapya watakapoaapishwa.
Hata hivyo Mbunge huyo ameleza mambo makubwa ambayo ameyafanya katika kipindi cha miaka mitano tangu achaguliwe kama mbunge viti maalumu ambapo ameeleza kuwa katika kipindi hicho ametumia Zaidi ya shilingi bilioni 11.7 katika masuala ya maendeleo ikiwemo kuchangia baadhi ya michango kuanzia ngazi ya kitaifa hadi ngazi ya kijamii pamoja na Sacco’s mbalimbali mkoani Kagera.
Kwaupande wake katibu mwenezi wa mkoa huo Ndg.Hamimu Mahamudu amesema kuwa chama hico kinawategemea wanawake na wakina mama katika kuhakikisha wanashinda uchaguzi mkuu ujao kwa mshikamano wao huku akiwasihi kuacha kupigana majungu na badala yake wanatakiwa kuwa wamoja.
Hamimu amesema kuwa katika kipindi ambacho wanawake wamependelewa na kupewa nafasi za uongozi basi ni kipindi cha serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli hiovyo wanaowajibu wa kuhakikisha chama chao kinashinda kwa wagombea wao kupata kura za kutosha, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuwaomba wakina mama hao kuhakikisha kata zote za manispaa ya Bukoba zilizokwenda upinzani zinarudi CCM pamoja na jimbo.
“Sisi kama chama tunatambua kuwa wanawake ni jeshi kubwa tena jeshi la ushindi, hivyo niwaombe wakina mama mkibebe chama hiki na kuhakikisha kinapata dola, katika mkoa wa Kagera Bukoba mjini ndiyo halmashauri pekee pamoja na jimbo ambavyo vimekwenda upinzani hivyo mnao wajibu wa kuhakikisha vyote vinarudi.” Ameeleza Mahamudu.
Aidha Ndg.Mahamudu amewakemea watia nia wanaopita na kuomba nafasi kabla ya muda huku wakitoa kashifa na majungu kwa wabunge na madiwani wanaomaliza muda wao kwa kusema hali hiyo haikubaliki nawote watachukuliwa hatua.
Amewatakla wagombea wagombee kwa utaratibu uliowekwa na chama chao na kuwasihi wagombea na wanaccm kwaujumla wake kujiepusha na vitendo vya Rushwa katika kipindi chote cha uchaguzi na kusema kuwa CCM haitawaacha salama wote watakaobainika.