Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kumuapisha Idd Hassan Kamanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni 2020.
………………………………………………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wote nchini kuimarisha mahusiano mazuri kazini ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kuwaapisha Mkuu wa mkoa wa Arusha, wakuu wa Wilaya wapya watatu(3) na wakurugenzi wapya wawili(2) walioteuliwa hivi karibuni.
Aidha Rais Magufuli amewataka viongozi hao kuzingatia viapo walivyo apa leo kuvitendea kazi ili kuleta maendeleo chanya katika maeneo yao ya kazi kwa kuwapa ushirikiano watendaji wao ili kufikia malengo chanya yanayotakiwa kwa watanzania.
“Nendeni mkafany kazi kwa uadilifu, kaitangaze sera ya serikali ya kuleta maendeleo kwa watanzania wote bila kuwa na ubaguzi katika utendaji wenu”, amesisitiza Rais Magufuli.
Pia Rais Magufuli amewaonya Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha na RPC wa Arusha kwa kuwataka kufanya kazi alizowatuma na sio kufanya kazi zisizo zao kama kutengeneza migogoro ya makusudi.
Naye Waziri WA Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ametoa wito kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kaishi vizuri na Ma DC wake , Wakuu wa Wilaya kufanya kazi kwa kuwaheshimiana na Mkuu wa Mkoa wao ili kuleta ushirikiano mzuri utakao leta matokeo chanya katika utendaji bora wa kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha.
“Mlioteuliwa kafanyeni kazi kwa ushirikiano mkubwa kila mtu amuheshimu mwenzake katika nafasi yake ili kufanyikisha shughuli za kimaendeleo katika maeneo yenu kwani tumepewa dhamana kubwa ya kumsaidia Mhe. Rais katika kuwatumikia watanzania hivyo tufanye kazi kwa mujibu wa katiba, sheria na taratibu za kazi zilivyo.
kama zinavyo tuelekeza.