*****************************
Dodoma, Juni 22, 2020
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Veterinari Na. 16 ya Mwaka 2003 amewateua Wajumbe wa Baraza la Veterinari Tanzania kama ifuatavyo: –
- Bhakilana Augustine Mafwere Mwakilishi Chama cha Wafanyabiashara wa Dawa za Wanyama
- Amandus Pachifius Muhairwa Mwakilishi, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
- Henry Budodi Magwisha Mwakilishi, Chama cha Madaktari wa Mifugo (TVA)
- Aloyce Edward Mbunito Mwakilishi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
- Emmanuel Bihemo Sokombi Mwakilishi, Madaktari wa Mifugo wa Sekta Binafsi
- Prof. Hezron Emmanuel Nonga Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
- Dkt.Ramadhani Abdul Mwaiganju Daktari wa Mifugo Mkoa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
- Bi.Trasila Claudio Kipesha Mwakilishi, Chama cha Wataalam Wasaidizi wa Mifugo (TAVEPA)
Uteuzi huu umeanza tarehe 21/6/2020 kwa kipindi cha miaka mitatu (3).
Aidha, Mwenyekiti wa sasa wa Baraza la Veterinari Tanzania, Prof. Rudovick Reuben Kazwala ataendelea na wadhifa huo hadi Mwezi Mei, 2021 kipindi chake cha miaka minne (4) kitakapomalizika.