Mkufunzi wa mafunzo hayo, Dk. Daniel Fussy akizungumza na vyombo vya habari.
Mkurugenzi wa HakiElimu nchini, Dk.John Kalage akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya walimu 40 wa elimu ya awali yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Mkwawa Iringa.
Baadhi ya walimu walioshirikia mafunzo ya kuwaongezea uwezo ikiwa ni Mradi huo uliopewa jina la Mwanzo Mzuri wa miaka tatu na unafadhiliwa na UKAid kupitia Mfuko wa Ustadi wa Maendeleo ya Binadamu na huletwa kwa kushirikiana na HakiElimu, Chuo Kikuu cha VIA Chuo Kikuu cha Denmark na Chuo Kikuu cha Mafunzo cha Mkwawa.
*********************************
NA DENIS MLOWE,IRINGA
WALIMU 40 wa shule za awali wamenufaika na mafunzo yenye lengo la kuboresha uwezo na weledi wa walimu kitaaluma na kivitendo yenye nia ya kuchochea zaidi matokeo ya kujifunza kwa wanafunzi wa awali.
Mafunzo hayo ambayo ni Mwanzo Mzuri inatarajia kuhakikisha kuwa vijana wa Kitanzania wataandikishwa elimu ya hali ya juu na salama ya mapema, ambayo inaboresha utayari wa shule na kuwasaidia kufikia ufikiaji wao kamili katika kujifunza kwa wanafunzi wa awali.
Mradi huo uliopewa jina la Mwanzo Mzuri ni wa miaka tatu na unafadhiliwa na UKAid kupitia Mfuko wa Ustadi wa Maendeleo ya Binadamu na huletwa kwa kushirikiana na HakiElimu, Chuo Kikuu cha VIA Chuo Kikuu cha Denmark na Chuo Kikuu cha Mafunzo cha Mkwawa ikiwa na mlengo wa kujaribu mfumo mpya wa ubunifu unaozingatia watoto kwa elimu ya mapema ambayo itaboresha utayari wa shule na matokeo ya kujifunza kwa watoto wa miaka 0-6.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa walimu hao, Mkurugenzi wa HakiElimu nchini, Dk.John Kalage alisema kuwa mradi huo umeigemea katika uwekezaji katika miundombinu ya matokeo bora ya kujifunza, pamoja na vyoo, usambazaji wa maji, vyumba vya madarasa au bustani za jikoni na kuwezesha jamii na maarifa na muundo wa kushiriki, na kuendesha suluhisho kwa maswala ya ECD, pamoja na elimu, ukatili dhidi ya watoto (VAC), afya, na lishe;
Aidha alisema kuwa mradi huo una lengo la kufuatilia utekelezaji wa sera na utetezi katika ngazi ya kitaifa na kitaifa kwa sera na miongozo itakayotoa elimu bora na ya awali ya msingi.
Dk. Kalage alisema kuwa mafunzo hayo ya Kozi ya Nne ya Mradi wa Mwanzo Mzuri yana umuhimu mkubwa sana katika kuboresha uwezo wa walimu katika kuwawezesha wanafunzi kujifunza na kuwawezesha na kuongeza weledi wa walimu kitaaluma na ki-vitendo, na hivyo kuchochea zaidi uwezekano wa kuboresha matokeo ya kujifunza ya wanafunzi..
Alisema kuwa Mpango huu ulikuwa ni sehemu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Wizara wa Kuendeleza na Kusimamia Walimu wa mwaka 2008 – 2013 (Teachers Development and Management Strategy (TDMS) ambapo mwaka 2017 Wizara ilitoa Mwongozo wa Mafunzo kazini kwa Walimu (National Framework For Continuous Professional Development Strategy for Practicing Teacher).
Alisema kuwa pamoja na jitihada hizi za Serikali sio walimu wote wamekuwa wakipata nafasi ya kujiendeleza wakiwa kazini kutoka na sababu mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti hivyo kama haki elimu kutokana na Utafiti wa “Mazingira ya Kujifunza na Kufundishia ya Elimu ya Awali’ tuliouzindua mwishoni mwa mwezi May 2020 una thibitisha haya.
Aliongeza kuwa kwa kutambua hilo HakiElimu kwa kushirikina na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa na Chuo Kikuu cha VIA cha Denmark vilibuni mafunzo haya kwa walimu wote 40 kupata mafunzo hayo ya awali kwa lengo la kuboresha elimu ya watoto wa awali.
“Tunatambua kuwa, serikali na wadau wengine pia wamekuwa katika jitihada za kuwapatia walimu mbalimbali hapa nchini mafunzo kazini. Hata hivyo, sisi tunaamini mafunzo haya yana sifa ya ziada maana yanalenga kuwapatia mbinu za kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa kuboresha matendo yenu mnapokuwa darasani. Ni wazi kwamba mwalimu anayejifunza nadharia kwa kuihusisha na vitendo halisi anakuwa na uwezo mkubwa zaidi katika ufundishaji na uambukizaji maarifa” alisema.
Aliongeza kuwa Mafunzo hayo yenye kozi tano ambazo zimeandaliwa katika mtiririko maalumu unaotegemeana ikiwemo umuhimu wa kufanya uchunguzi na uandishi wa taarifa ambazo zitasaidia katika utendaji wenu wa kila siku, michezo na Kujifunza ikiendana na Mtaala wa Elimu ya awali unaosisitiza matumizi ya mbinu ya michezo katika kufundisha na kujifunza.
Aidha mafunzo yaliyotolewa yalilenga kukuza uwezo wa wanafunzi kujifunza kwa kushirikiana ili kuwawezesha wanafunzi kufikia malengo kwa pamoja na kupunguza mashindano na utengano na kozi nyingine kujenga uwezo wa kuwasaidia watoto kutumia viungo vyao kutambua na kujifunza
Dk.Kalage alitoa wito kwa walimu hao kubuni au kupendekeza mbinu muafaka za kukabiliana na changamoto ya kufundisha madarasa makubwa na eneo la pili lenye changaamoto, ni utekelezaji wa elimu jumuishi ambapo serikali imeweka msisitizo mkubwa kupitia sera na mipango mbalimbali ya elimu.
Alisema kuwa kwa upande wao Ujumbe wa HakiEli elimu ya awali ina umuhimu mkubwa sana kwa kuwa ndiyo msingi wa wanafunzi bora vyuoni na viongozi na watendaji mahiri hapo baadae hivyo tunapaswa kuipa umuhimu unaostahili na kila mmoja ni muhimu kuzingatia nafasi yake katika hili.
Aliongeza kuwa vyuo ni lazima vijikite na viazimie kuzalisha walimu bora na watendaji bora watakaosimamia elimu ya awali na Walimu ni lazima wazingatie mafunzo na wayatumie ipasavyo kuwaandaa watoto na serikali ni lazima iweze kuwaunganisha na kuwatengenezea mazingira wezeshi wadau wote wa elimu ya awali zikiwemo shule
Kwa upande wake, Mkufunzi wa mafunzo hayo, Dk. Daniel Fussy kutoka chuo kikuu cha Mkwawa, alisema kuwa katika mafunzo ya awali waligundua kuwa kulikosekanika muungano kati ya walimu na wanafunzi hivyo mafunzo hayo yamewasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto hiyo.
Alisema kuwa walimu wanatakiwa pindi wanafundisha muhimu sana kufanya uchunguzi kwa watoto na kubaini talanta walizonazo na kutowaacha peke yao pindi mafunzo yoyote yanapoendelea hivyo lazima kuandika taarifa kubaini mapungufu ya wanafunzi wa awali kwa lengo la kuwasaidia.