Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akikagua moja ya vitendea kazi vilivyopo katika kituo cha Wazee wasioniweza Fungafunga mjini Morogoro. Kulia ni Afisa Mfawidhi wa Kituo hicho Rehema Kombe.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akimsikiliza Lucy Kambilo mmoja wa wahudumu katika kituo cha Wazee wasioniweza Fungafunga mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akikagua shamba la mchicha linalolimwa na wazee wasiojiweza wanaoishi katika kituo cha Fungafunga mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na watumishi wa Kituo cha Wazee wasiojiweza Fungafunga mjini Morogoro.
Baadhi ya Wazee wasiojiweza wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu wakati alipofanya ziara kukagua huduma zinazotolewa katika kituo cha kulea wazee wasiojiweza Fungafunga mjini Morogoro.
Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Wazee na Wasiojiweza FungaFunga Morogoro Rehema Kombe akieleza namana wanavyotoa huduma kwa wazee wasiojiweza katika kituo hicho wakati Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu wakati alipofanya ziara kukagua huduma zinazotolewa hapo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akimkabidhi Asha Selemani mmoja wa Wazee wasiojiweza wanaoishinkatika kituo cha Fungafunga mjini Morogoro.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiiano Serikalini WAMJW
……………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu, Morogoro.
Wazee wanaoishi katika kituo cha makazi ya Wazee Wasiojiweza cha Fungafunga Mkoani Morogoro wamempongeza Rais, Dkt. John Magufuli kwa kazi iliyotukuka tangu alipoingia madarakani ikiwa ni pamoja na kuboresha makazi na huduma kwa wazee Wasiojiweza.
Pongezi hizo zimetolewa mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu alipofanya ziara kituoni hapo kukagua uendeshaji na huduma zinazotolewa kwa Wazee.
Baadhi ya Wazee Waliopata fursa ya kuzungumza, wamesema Serikali ya awamu ya tano imewaboreshea huduma na kwamba Afya zao zimeimarika ikilinganishwa na kipindi kilichopita.
Mzee Joseph Kaniki alisema katika uongozi wa Serikali ya awamu ya tano, Wazee wametambulika na kuthaminiwa kutokana na huduma nzuri wanazozipata kituoni hapo na hivyo kuwafanya kunawiri.
“Mhe. Katibu unavyoona tunanawili hivi ni kwasababu tunatunzwa na tunakula vizuri, Mwenyezi Mungu azidi kuwalinda na kuwatunza, Rais Wetu, Mawaziri, Wewe Katibu wetu unayetutembelea kila mara pamoja na Mama yetu Mlezi” alisema
Mzee Abdallah Mbena maarufu kama Chalinze alisisitiza kuwa wazee waishio katika vituo hivyo watakumbwa na kifo kwa Mipango ya Mwenyezi Mungu lakini sio kwa kukosa huduma za kijamii.
Kwa upande wake, Mhudumu wa Afya Mkuu katika makazi hayo ya wazee, Elizabeth Mandelu alisema Rais Dkt. Magufuli kuwa ni tunu kwa Watanzania kutoka kwa Mungu huku akitoa mfano kwa alivyowatia moyo Wananchi wake hadi kupungua kwa ugonjwa wa COVID 19.
“Kwanza nikiri kwamba ugonjwa huu umeondoka kwa muujiza wa Mungu, lakini pia tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Rais Magufuli kama zawadi ambaye kwa ujasiri mkubwa ametutia shime sisi Watanzania kukabiliana na ugonjwa huu wa Korona” alifafanua.
Akitoa maelezo ya uendeshaji wa makazi ya Wazee Fungafunga, Afisa Mfawidhi wa Kituo hicho Rehema Kombe aliipongeza Serikali kwa kuwajali na kuwatunza Wazee huku akifafanua makazi hayo ni nyumbani na sio mabweni kama ilivyotafsiriwa na wengi.
Ameongeza kuwa makazi hayo yanahitaji kuboreshwa zaidi kwa kujengewa bwalo la chakula, ukarabati wa jiko na majengo mbalimbali yanayotumika kwa miradi inayoendelea kwenye makazi hayo.
Kabla ya kupokea taarifa ya juu ya uendeshaji wa makazi, Katibu Mkuu Dkt. John Jingu alipata fursa ya kukagua miradi mbalimbali inayoendeshwa katika makazi hayo na kupata taarifa kutoka kwa baadhi ya wazee wanaojishughulisha na kazi ya mikono na kilimo cha mboga mboga.
Akizungumzia hali ya Wazee kituoni hapo, Dkt. Jingu amesema kufanya kwao kazi ni mfano wa kuigwa kwa vijana ambao wakati mwingine wanabaki katika makundi sogozi bila kuwa na shughuli maalum ya kufanya.
“Nyie mmefanya kazi mnalima na mimeona Bustani, mchicha umestawi vizuri kabisa. Vijana wanaoshinda bila kazi wanatakiwa kuinga mfano kwenu”
Pia ameishukuru Serikali kuanzia ngazi ya Mtaa hadi taifa kwa ushirikiano unaolenga kuleta utatuzi wa matatizo katika jamii huku akifafanua kuwa viongozi katika ngazi zote wanalenga kumsaidia Rais, Dkt. John Mafuguli katika kuleta maendeleo kwa Watanzania.
Serikali inendelea kutoa huduma za Msingi chakula, mavazi, malazi na matibabu kwa Wazee wasiojiweza hutolewa katika makazi kumi na matatu yanyomilikiwa na Serikali ambayo ni Kibirizi, Njoro, Kolandoto, Bukumbi, Ipuli, Fungafunga, Mwanzange, Misufini, Nunge, Nyabange, Kiilima Sukamahela na Magugu.