Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Urais kwa Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM White House Dodoma leo tarehe 17 JUNI 2020.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Makao Makuu ya CCM White House Dodoma leo tarehe 17 JUNI 2020 mara baada ya kuchukua Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais kwa Tiketi ya CCM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachama wa CCM katika Makao Makuu ya CCM White House Dodoma leo tarehe 17 JUNI 2020 mara baada ya kuchukua Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais kwa Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Ofisi ya CCM Makao Makuu ya Mkoa Dodoma mara baada ya kupata wadhamini wa Chama chake cha Mapinduzi CCM. PICHA NA IKULU
*******************************
Mwenyekiti wa @ccm_tanzania Dkt @MagufuliJP leo Juni 17, 2020 amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chake cha CCM. Fomu hiyo amekabidhiwa na Katibu Mkuu Dkt Bashiru Ally asubuhi hii jijini Dodoma.