![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/IMG_2982-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/IMG_2986-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/IMG_2991-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/IMG_3023-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/IMG_3064-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/IMG_3026-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/IMG_3051-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/IMG_3004-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/IMG_3081-1024x682.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/IMG_3082-1024x682.jpg)
………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna, Dodoma
Serikali imeitaka sekta ya kilimo cha umwagiliaji nchini kuhakikisha miradi yote ya umwagiliaji nchini inaendeshwe kibiashara ili kurudisha mitaji na kupanua eneo la uwekezaji.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba, jijini Dodoma, wakati akizungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya umwagilijai nchini (NIRC).
Mhe.Mgumba amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne serikali imewekeza kiasi cha Sh. bilioni 96, katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji nchini lakini hakuna mapato ambayo serikali inayapa kutokana na miradi hiyo.
“Hivyo ni wakati sasa miradi yote ya umwagiliaji nchini, kuanza kuendeshwa kibiashara ili kurudisha mitaji mikubwa iliyowekezwa na serikali na kupanua eneo la uwekezaji huo katika sekta hiyo nchini”, ameeleza Mhe. Mgumba.
Aidha Mhe.Mgumba amesisitiza kuwa miradi ya umwagiliaji ndiyo ambayo imebakia kuwa sehemu ya serikali kuwekeza fedha bila kupata mapato hivyo sasa ni lazima tume ya Taifa ya umwagiliaji kuona namna ya kuendesha miradi hiyo kibiashara.
“Miradi hii inatumia fedha nyingi sana za uwekezaji kutoka serikali kuliko miradi mingine, lakini hakuna kiasi chochote ambacho serikali inakipata kwa hivi sasa, ukiangalia hata kwenye miraddi ya vituo vya afya pamoja na kuwa ni ya jamii lakini watu wanachingia, kumuona daktali tuu ni Sh. 8,000 au 10,000”amebainisha Mhe.Mgumba
Vilevile Mhe. Mgumba amesema kuwa bila miradi hiyo kuendeshwa kibiashara mtiririko wa ukuaji wa sekta hiyo utayumba kwani wawekezaji watakimbilia kwenye miradi inayo rudisha faida.
“Kama mradi tumewekeza bilioni tatu, tukipata faidi basi tutakwenda kuwekeza katika maeneo mengine ili kuwa na kilimo cha uhakika ambacho hakitegemeo maji ya mvua kwa asilimia 100, na kuongeza uchumi wetu, kuongeza pato la taifa pampja na kuwa na uhakika wa chakula ili kumpiga adui umaskini”ameongezea Mhe.Mgumba
Mhe. Mgumba amesisitiza kuwa ni lazima miradi yote ya umwagilijai ambayo serikali imewekeza kukusanya mapato angalau kwa asilimia tano ya mapato kwani mpaka sasa hakuna kilicho kusanywa.
“Ukizingatia miradi hii ni ya kiuchumi lazima tukusanye kitu, kwani hata miradi ile ambayo ni ya kijamii kama hospitali, barabara inatushinda katika uchangiaji wa mapato ya serikali hivyo ndugu zangu wa tume lazima tubadilike lazima tupate mwongozo haraka utakao tuweza kuyafanya haya”ameweka wazi Mhe. Mgumba.
Mgumba amesema kabla ya mwezi Julai mwaka huu, lazima kuwe na mfuko wa umwagiliaji pamoja na mwongozo wake utakao saidia katika uboresha sekta hiyo nchini.
Naye Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji nchini Daudi Kaali, amesema kuwa hali ya kilimo cha umwagiliaji nchini, Tanzania ina hekta milioni 29.4 zinazofaa kwa kilimo hicho.
“Kati ya hekta hizo, hekta milioni 2.3 zina uwezekano mkubwa wa kumwagiliwa, hekta milioni 4.8 zinauwezekano wa kati na hetka milioni 22.3 zinauwezekano mdogo wa kumwagiliwa”ameeleza Kaali.
Kaali amesema kuwa kufikia mwaka 2015, kabla ya kuanza kwa tume ya umwagiliaji jumla ya hekta 461,000 zilikuwa zimeendelezwa kwa kilimo cha umwagiliaji.