Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi akimpa pole Fundi Ujenzi, Daniel Michael wa Kijiji cha Itagata baada ya kutoa malalamiko ya kutolipwa zaidi ya Sh.milioni 4.6 na mkandarasi aliyejenga bwawa la mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika kijiji hicho, wakati akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi juzi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dk. Angelina Lutambi, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Itigi (hawapo pichani katika ziara hiyo. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni, Jumanne Makhanda, akizungumza.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, John Mgalula, akizungumza.
Mhandisi anaye simamia mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Kijiji cha Itagata, Sembua Mrisha, akizungumza.
Moja ya mfereji wa maji katika mradi huo.
Safari ya ukaguzi wa miradi ikiendelea. Kulia ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Manyoni, (OCD) Charles Kidesheni.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Ally Minja akizungumzia mradi wa maji wa vijiji sita.
Ukaguzi wa mradi wa maji wa vijiji sita ukifanyika.
Ukaguzi wa jengo la Zahanati ya Kijiji cha Kamnyanga ukifanyika.
Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Aghondi, Frida Mhango, akitoa taarifa ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kamnyanga.
Mkutano na Wananchi wa Kijiji cha Kamnyanga ukiendelea.
Bwawa la mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa kijiji hicho Itagata.
Shamba la Mpunga la Kijiji cha Itagata. Mkutano Kijiji cha Kamnyanga ukiendelea.
Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Kamnyanga ambao ujenzi wake unaendelea.
Shamba la Korosho la Kijiji cha Kamnyanga.
Mwenyekiti wa Shamba la Umwagiliaji la Kijiji cha Itagata, Salum Mayunga (Fupe) akizungumza.
Makamu Mwenyekiti wa Shamba la Umwagiliaji la Kijiji cha Itagata, Rehema Shadrack akizungumza.
Mkulima Juma Ramadhani akiendelea na kazi katika shamba la kilimo cha umwagiliaji la kijiji hicho.
*********************************
Na Dotto Mwaibale, Itigi Singida.
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk.Rehema Nchimbi amesema ni wajibu wa Serikali kulinda haki za raia na mali zao.
Nchimbi aliyasema hayo juzi wakati akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa fundi ujenzi, Daniel Michael wa Kijiji cha Itagata ambaye alidai hajalipwa zaidi ya Sh.milioni 4.6 na mkandarasi aliyejenga bwawa la mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa kijiji hicho.
Awali fundi huyo aliinua bango la madai hayo kabla Dk.Nchimbi hajaanza kuzungumza na wananchi kuhusu mradi huo.
Nchimbi alisema kwamba hata siku moja Serikali haiwezi kuona inashangilia, inafurahia matokeo makubwa na kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi kwa ujenzi wa miradi mikubwa namna hiyo alafu kukawa na wananchi walioshiriki kufanya kazi hizo hawapati haki zao.
Mkuu huyo wa mkoa aliagiza hadi ifikapo Juni 28, 2020 wawe wamelipwa fedha hizo.
” Mkurugenzi, RAS ninaagiza walipwe kutoka katika fedha Rentetion Money ile fedha ya mkandarasi ambayo inatunzwa kwa ajili ya kipindi cha matazamio ya mradi huo” alisema Nchimbi.
Akizungumzia mradi wa shamba la mpunga linalolimwa kwa kilimo cha umwagiliaji katika kijiji hicho alisema Serikali imewekeza fedha nyingi ambapo aliwataka wasimamizi kuongeza uzalishaji ili kwenda sanjari na thamani halisi ya shamba hilo.
Aidha Dk.Nchimbi akizungumzia upanuzi wa ekari 16 za wananchi 16 katika shanba hilo, ambao kila mmoja wao ana watu watano alisema ni wa muhimu na haupaswi kuchelewesha hivyo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo John Mgalula kutoka Sh.milioni 1.5 zilizokuwa zikihitajika ambapo alisema tayari zilikuwa zimekwisha tolewa.
Akizungumzia mradi wa kilimo cha shamba la korosho lililopo Kijiji cha Kamnyanga alitoa angalizo kwa mkurugenzi wa wilaya hiyo kuchukua tahadhari ya fedha zitakazo kuwa zikotolewa na wananchi.
Katika hatua nyingine Dk. Nchimbi alisema changamoto ya kuwepo kwa tembo wahalibifu wa mikorosho katika shamba hilo isiwakatishe tamaa kwani hata Mikoa ya Mtwara na Lindi kuna misitu mikubwa yenye tembo wengi lakini zao hilo limekuwa likilimwa kwa mafanikio makubwa.
Akisoma taarifa ya mradi huo, Afisa Kilimo wa Kata ya Ighonda, Christina Buluba, alisema ulibuniwa na wananchi wa kijiji hicho kwa lengo la kuwa na zao la kudumu na kujiongezea kipato.
Alisema shamba hilo lina jumla ya ekari 1, 484 ambalo zimepandwa jumla ya mikorosho 41,608 na kuwa wadau wa kilimo hicho cha pamoja (Block Farming) wanatoka ndani ya kijiji na halmashauri hiyo.
Akikagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kamnyanga ambao umefikia hatua ya upauaji aliagiza uongozi wa wilaya hiyo kufanya tathmini ya gharama halisi ya mradi huo kama unalingana na Sh.milioni 33 alizotajiwa wakati akipokea taarifa.
Akizungunzia mradi wa maji wa vijiji sita vya Songambele, Mlowa, Tambukareli, Majengo, Ziginali na Itigi uliopo katika halmashauri hiyo alisema wananchi hawahitaji kujua ni shilingi ngapi zimetumika bali wanataka kuona kitu ambacho wanaweza kukisema kuwa ni hiki.. hata wakitaka kusema asante kwa Rais John Magufuli kwa kuwapelekea mradi huo mkubwa wa maji wawe na tafsiri yao na si vinginevyo.