Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Plc wakishiriki kupanda miti patika ene la kiwanda cha Bia cha Ilala mwishoni mwa wiki
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Plc wakijiandaa kuanza zoezi la upandaji miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2020
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Plc katika picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2020.
……………………………………………………………………………..
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL Plc) mwishoni mwa wiki walishiriki kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2020, iliyoadhimishwa Juni 4 kwa vitendo ambapo walishiriki kupanda miti kuzunguka eneo la kiwanda chao cha Ilala jijini Dar es Salaam sambamda na kupatiwa mafunzo kutusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira.