Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwa amenyanyua mkoba wa Bajeti Kuu ya Serikali, ya mwaka 2020/2021 Bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha bungeni jijini Dodoma Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2020/2021 ambapo Serikali imepanga kukusanya na kutumia takribani shilingi trilioni 34.9 kwa matumizi ya maendeleo na matumizi mengine.