………………………………………………………………….
Naibu Waziri Kilimo Mhe.Hussein Bashe leo amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw.Michael Dunford Ofsini kwake ambapo walifanya mazungumzo mafupi.
Wakiwa katika kikao hicho kifupi Bw.Michael amesema ujio wake umelenga kuagana na uongozi wa wizara kwa niaba ya wafanyakazi wote kwa kuwa amepangiwa kazi nyingine ya kuwa Mwakilishi wa WFP katika nchi za Afrika mashariki ambapo makao makuu yake yapo jijini Nairobi Nchini Kenya.
Bw. michael ameleza kufurahishwa na utendaji kazi wa serikali kupitia wizara ya kilimo ambapo miradi mingi chini ya WFP ilitekelezwa kwa ufanisi mkubwa.
Pia amemshukuru Mhe.Bashe kwa namna wizara walivyoweza kushirikiana naye wakati wa uongizi wake ambapo amekiri kwamba ushirikiano huo ulisababisha kutekeleza majukimu yake kwa ufanisi zaidi alisema Bw.Michael.
Naye Naibu Waziri Kilimo Mhe. Bashe mara baada ya shukrani hizo amemuomba Bw. michael kufikisha ujumbe Wfp kwamba waongeze wigo wa ununuzi wa mazao ya kilimo nchini hapa yakiwemo mtama na ngano badala ya mahindi peke yake ili wakulima waweze kupata fursa nyingine ya soko la mazao hayo.
“Tumekuwa tukifanya biashra na WFP hasa ya mazao ya mahindi kwa muda sasa kupitia wakala wa uhifadhi wa Chakula nchini NFRA jambo ambalo limesaidia kuongeza soko na ubora wa mahindi kwa wakulima lakini tunadhani sasa muongeze wigo katika kununua mazao mengine kama ngano na mtama kwakuwa mahitaji yake ni makubwa,, alisema Mhe. Bashe.
Aidha Mhe.Bashe alimalizia kwa kusema kwamba Wizara ya Kilimo itaendelea kushirikiana na Shirika hili kwa kuwa wamekuwa wadau wakubwa katika kushughulikia masuala muhimu ya usalama wa Chakula na lishe katika taifa letu.