Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akizindua rasmi eneo maalumu la kunawa mikono kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Msalato jijini Dodoma. Eneo hilo linahudumiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma, ni moja ya hatua za Wizara ya Maji katika kusaidia jamii na wadau wake katika kujikinga na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID 19).
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo (kulia) akinawa mikono, katika eneo maalum la kunawa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Msalato, mara baada ya kuwakabidhi eneo hilo jijini Dodoma. Wengine ni viongozi alioambatana katika hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Msalato baada ya kuwakabidhi eneo la kunawa mikono na vitakasa mikono vilivyozalishwa na wizara yake. Vitakasamikono hivyo
vimetolewa kwa wanafunzi, pamoja na walimu wanaowafundisha wakiwa katika maandalizi
ya Mtihani wa Kidato cha Sita.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo, pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Msalato Bi. Neema Maro na wanafunzi wa Kidato cha Sita wanaojiandaa kwa mtihani wa wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya eneo la kunawia mikono walilokabidhiwa na Wizara ya Maji shuleni hapo.
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akisoma maelezo ya moja ya Kitakasa mikono kilichozalishwa na wataalam wa wizara yake kabla ya kugawa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Msalato jijini Dodoma. Wanafunzi hao ni miongoni mwa wanafunzi wanaojiandaa na mtihani wa Kidato cha Sita. Anayetizama ni Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji, Wizara ya Maji Bw. Phillipo Chandy anayeongoza idara iliyozalisha vitakasa mikono.
Mkurugenzi wa Idara ya Ubora wa Maji, Wizara ya Maji Bw. Phillipo Chandy akionyesha Kitakasamkono kinavyofanya kazi kwa kupuliza (spray) kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo. Vitakasamikono vimegawiwa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msalato wanaojiandaa na Mtihani wa Kidato cha Sita.