***********************************
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda aameipongeza Wilaya ya Temeke kwa kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Amezungumza hayo leo wakati akikagua miradi ya maendeleo wilayani humo ikiwemo mfereji wa maji katika shule ya Kibasila,hospitali zilizopo yombo vituka na buza pia madarasa katika shule ya Sekondari Mbagala.
Pia amempongeza mkuu wa Wilaya hiyo kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa 124, madawati 7179 na matundu ya choo 124.
Vilevile amesema Wilaya ya Temeke inastahili kuwa shujaa na inastahili kupongezwa kwa kazi walioifanya.
Sanjari na hayo Rc Makonda amesema tareha 20 mwezi wa sita atapita kukabidhi miradi ya maendeleo kwa viongozi wa Chama akiambatana na kamati ya Siasa mkoa.
Hata hivyo Rc Makonda amemalizia kwa kuwataka wananchi wamruhusu Mh Rais Dk John Magufuli afanye kampeni kiwilaya ili apate muda wa kupumzika na amewataka wazazi kuwachunga watotowao ambao wanatabia ya udokozi.