Rais Mhe.Dkt. John Magufuli akiwasili katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania unaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi mbalimbali.
Rais Mhe.Dkt. John Magufuli akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania unaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ambao unafanyika kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi mbalimbali.
Katibu Mkuu wa CWT Deus Seif,akitoa taarifa katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania unaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi mbalimbali.
Sehemu ya wajumbe kutoka mikoa mbalimbali wakifatilia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania unaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi mbalimbali.
…………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
RAIS Mhe.Dkt. John Magufuli amesema kuwa karibuni shule za Awali, Msingi na Sekondari zitafunguliwa baada ya kuona hali ya ugonjwa wa Corona inavyoendelea kupungua nchini.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania unaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, amesema kuwa serikali ipo mbioni kufungua shule kwani anajua walimu wa Tanzania wanapenda kufanya kazi.
Mhe.Rais Magufuli amesema kuwa taarifa alizopata juzi kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kuwa mpaka juzi kulikuwa na wagonjwa wanne kutoka Dar es Salaam, hivyo hali ya ugonjwa inapungua.
“Walisema kwa Afrika maiti zitazagaa ila Mungu wetu anatupenda, Taifa hili tulifanya maombi siku tatu na juzi Dar es Sala niliambia kuna wagonjwa wanne …uzushi utatolewa wa kila aina ila leo naona walimu hapa hamjavaa barakoa,” Ameleza
“Nashukuru Mungu na Watanzania, tumeshinda na tukaendelee kushinda, nina hakika hivi karibuni baada ya kufungua vyuo, tunaangalia mambo yanavyoenda na shule za msingi na chekechea nazo ziko mbioni tutazifungua ili walimu wakafanye kazi,
“Hapa tunaonana nilikuwa namuangalia Spika Job Ndugai akiwa anaongoza Bunge yupo pekee yake kwenye kiti chake lakini kavaa barakoa hivyo tumtangulize Mungu katika hili,” amesema Rais Magufuli
Hata hivyo amesema kuwa mtu yeyote akikuletea barakoa kataa mwambie akavai yeye na mtoto wake na mke wake bora mtu akaamua kushona barakoa yake mwenyewe kuliko kuchukua barakoa ambayo haijulikani imetoka wapi.
”Yaani nashangaa kuna group linajiita Magufuli Forum mimi hata silijui nimewaona wakigawa barakoa wanatoa wapi hivyo naagiza viongozi wa mikoa na wilaya wakiona mtu anagawa barakoa wamuulize katoa wapi na wapi zimedhibitishwa”Ameeleza
Nawaomba kila mtanzania achukue tahadhari tusidanganywe kwa kuletewa barakoa sijui wametoa wapi, naamini ugonjwa huu utapungua tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu.
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania wa leo ni kwa ajili ya uchaguzi wa kuchagua viongozi mbalimbali Rais,Makamu wa Rais,Katibu Mkuu,Naibu Katibu Mkuu pamoja na Mweka hazina.