*************************
Dar Es Salaam, 20/06/2019
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amesema kuwa hakuna matishio
yoyote ya kigaidi nchini na kwamba jeshi la Polisi lipo imara katika
kuhakikisha usalama wa raia na mali zao na kwamba wananchi waendelee
kutimiza wajibu wao ikiwa pamoja na kujenga uchumi wa nchi.
IGP Sirro amesema hayo kufuatia taarifa inayosambaa mitandaoni kuwepo
kwa shambulio la kigaidi na kuwatia hofu wananchi juu ya usalama wao.
IGP Sirro amesisitiza kuwa hadi sasa hakuna tishio lolote la kigaidi na
kuwataka wananchi kutumia mitandao ya kijamii kwa faida na si
kuwajengea hofu wananchi.