Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020 vilivyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli mkoani hapa jana. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson Masaka vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa akiwa na viongozi wenzake wa wilaya hiyo baada ya kupokea vitambulisho hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri , akiwa na viongozi wenzake wa wilaya hiyo baada ya kupokea vitambulisho hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akiwa na viongozi wenzake wa wilaya hiyo baada ya kupokea vitambulisho hivyo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Justice Kijazi, Afisa Biashara, Sigisberto Mwacha na Katibu Tawala, Winfrida Funto.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson Masaka, akiwa na viongozi wenzake wa wilaya hiyo baada ya kupokea itambulisho hivyo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, akiwa na viongozi wenzake wa wilaya hiyo baada ya kupokea itambulisho hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akimkabidhi Mjasiriamali, Prisca Nyelo kutoka Bhigizimana Product kitambulisho chake cha Ujasiriamali Awamu ya pili 2020.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi amewataka maofisa wa Serikali watakao kuwa wakigawa vitambulisho vya Wajasiriamali Awamu ya pili 2020 vilivyotolewa na Rais John Magufuli kuwa waaminifu na waadilifu.
Dkt.Nchimbi alitoa ombi hilo jana wakati akiwakabidhi vitambulisho hivyo wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Singida.
“Rais John Magufuli mwaka huu tena ametuletea vitambulisho hivi pamoja na malengo mengine vinadhihirisha kwamba Tanzania wananchi wake wote wanafanya kazi katika ngazi mbalimbali wakiwamo wajasiriamali na kuwa hakuna zuio la kutofanya kazi wakati huu wa kipindi cha Covid-19” alisema Nchimbi.
Dkt.Nchimbi alimpongeza Rais Magufuli kwa malezi yake ya kipekee kwa Watanzania na hatua aliyoichukua kukabiliana na Corona.
Alisema Tanzania hivi sasa tupo katika safari ya kuelekea uchumi wa kati wa viwanda ukiwepo Mkoa wa Singida hivyo vitambulisho hivyo vitatoa fursa zaidi kwa wajasiriamali kutambulika.
Dkt. Nchimbi alisema vitambulisho hivyo vimewafanya wajasiriamali kuthaminiwa, kutambuliwa, kuwa na haki na fursa ya kushiriki kufanya biashara pamoja na kuiamini Serikali yao.
Alisema kabla ya Rais Magufuli ajaanzisha utoa wa vitambulisho hivyo wajasiriamali walikuwa hawathaminiwi bidhaa zao zilikuwa zikiharibiwa na hawakuwa na uwezo wa kuratibu mipango ya biashara zao lakini leo hii wanaheshimika na hakuna tena zile tozo walizokuwa wakizitoa ambapo kwa mwaka zilikuwa ni nyingi tofauti na sasa.
Aliongeza kuwa vitambulisho hivyo vitakuwa vikitambulika kila wilaya kwa namba maalumu na mjasiriamali atalipia sh.20,000 kwa njia ya mtandao na fedha hizo zitaingizwa kwenye mfumo wa upokeaji wa fedha za Serikali tofauti na ilivyokuwa mwaka jana ambapo kila mtu aliweza kupokea fedha hizo toka kwa mjasiriamali hivyo kuleta changamoto ya utunzaji wa fedha hizo.
Dkt.Nchimbi alisema vitambulisho vilivyotolewa kwa awamu ya kwanza ni 9,000 kati ya vitambulisho 55,000 vitakavyotolewa kwa wajasiriamali wote wa Mkoa wa Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungu, Edward Mpogolo alisema vitambulisho hivyo vya awamu ya kwanza katika wilaya hiyo wajasiriamali walichangia zaidi ya sh.milioni 100 na kuwa kwa awamu hii ya pili wamepanga kuwafikishia katika magulio yote, na kila maeneo walipo wafanyabiashara, masokoni na kwa wauza nguo.