…………………………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh. Adam Malima amewaagiza maafisa wa Forodha katika kituo cha Silali kuhakikisha kuwa madereva wa malori ya mizigo hawaingii nchini kupitia Mpaka huo badala yake washushe mizigo yao kwenye mpaka huo kwaajili ya kufaulishwa tayari kuingia mkoani Mara.
Mh. Malima amesema kuwa uamuzi huo unatokana taarifa zinazotolewa kutoka nchi jirani ya Kenya zikidai kuwa maderava wanaotoka Tanzania kuingia Kenya wengi wao wana ugonjwa wa corona jambo ambalo alidai kuwa lina utata hivyo ni vema na wao pia madereva wao wasiingie nchini kupitia mpaka huo.
Amesema kuwa kuanzia sasa magari hayo ya mizigo yatalazimika kushusha mizigo mpakani hapo na wenye mizigo kuifaulisha katika magari ya Tanzania ili kuepuka muingiliano wa madereva kutoka Kenya na kuja nchini.
Amesema kuwa serikali ya Tanzania haina shida na maamuzi ya nchi ya Kenya kufunga mipaka yake kwavile nchi hiyo ni nchi huru yenye uwezo wa kufanya maamuzi yoyote juu ya mipaka yake na kwamba Tanzania na Kenya ni marafiki na ndugu hivyo hakuna