| Ukaguzi wa Tanki la Maji eneo la Muriet lenye ujazo wa lita milioni 200 picha zote na Ahmeid Mahmoud Arusha. Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amezitaka halmashauri zote mkoa wa Arusha kuhakikisha zinafunga vifaa vya Afya kwenye hospitali na vituo vya Afya sanjari na wakandarasi wa Mradi mkubwa wa maji wanaendelea na kazi za Ujenzi wa miradi hiyo usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Maji kwenye mkoa huo kama ilivyopangwa kabla ya August. Gambo ametoa Agizo hilo Jana ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tatu kukagua Miradi ya maji na Afya kwenye halmashauri saba za mkoa huo ambapo amesema kuwa suala hilo halihitaji kungojewa hivyo hatua zinahitajika kuchukuliwa haraka na atakuwa anafuatilia kila mara ili wananchi wapate huduma. Amesema kuwa msingi wa ujenzi huo ambao fedha zipo na zimeshatolewa hivyo kila moja achukuwe hatua kuhakikisha serikali inatekeleza miradi kwa wakati ili ifikapo mwezi wa nane wananchi wawe wanapata huduma za maji na Afya ilikuwaondolea adha ya ukosefu wa huduma hizo. “Nimetembea maeneo mengi kwenye sekta ya afya nimegundua vifaa tiba ikiwemo kwenye maabara na vyumba vya Upasuaji haijafungwa natoa agizo vifungwe haraka ili wananchi wapate huduma za afya sanjari na huduma za maji mkasimamie kuhakikisha wanamaliza ndani ya muda wa mkataba na kujenga miradi hiyo kwa usiku na mchana kabla ya mwezi wa nane na ikikamilika ianze kazi mara moja” Kwa Upande wake Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni wameahidi kusimamia maagizo yote yaliotolewa na mkuu wa mkoa ili kuona wananchi wanapata huduma hizo kwa muda uliopangwa. |