Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo akitoa maelekezo katika eneo la ujenzi wa Hospital ya Uhuru inayojengwa
katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
*********************
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani
Jafo(Mb) ameagiza ujenzi wa Hospital ya Uhuru uanze Wiki ijayo Tar.24/06/2019 ili kutimizia ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Dec, 2018 na kuelekeza fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
Waziri Jafo alitoa maagizo hayo wakati wa ziara yake Wilayani Chamwino kukagua
ujenzi wa hospital hiyo ya kisasa na kukuta hakuna ujenzi ulioanza na hata eneo hilo halijasafishwa.
Akizungumza katika ziara hiyo Jafo amesema hataki kusikia hadithi zozote
zinazokwamisha kuanza kwa ujenzi wa Hospital ya Uhuru kwa sababu Agizo lilishatoka na fedha zilishatengwa.
“Sikutarajia kukuta eneo la ujenzi likiwa katika hali hii, hakuna kitu kilichofanyika mpaka leo halafu mnaniambia bado mnaendelea na vikao sijui mnajadili nini ambacho hakiishi ninachotaka kuona hapa ni ujenzi kuanza mara moja yaani ikifika Jumatatu hali ya hapa iwe tofauti mkamilishe mambo yote yanayotakiwa kwa siku hizi chache na kazi hii ianze”
Waziri Jafo aliongeza kuwa nimesikia bado mnajadili kuhusu ramani gani itumike katika ujenzi huu sasa naagiza ujenzi wa Hospital hii utumie ramani ya Hospital ya Tunduma ambayo ni Gorofa kwa sababu ramani ile itasaidia katika matumizi bora ya Ardhi na pia itakidhi mahitaji ya kuwa na jengo la kisasa lenye hadhi ya Hospital ya Uhuru.
Wakati huo huo Waziri Jafo aliagiza kikosi maalumu cha SUMA JKT kitumike katika
ujenzi wa hospital ya Uhuru ili iweze kwenda na muda na ubora uweze kuzingatiwa na Wakala wa Majengo (TBA) watumike kama washauri na wadhibiti Ubora wa Majengo ya Hospital hiyo.
“Natoa miezi sita ujenzi wa Hospital hii uwe umekamilika na ndio maana nikaagiza
Kikosi cha Jeshi SUMAJKT kitumike ili tuweze kwenda na muda kwahiyo ifikapo Dec, 2019 nataka kuja kuona majengo yote ya Hospiatl yakiwa yamekamika na kwa ubora wa hali ya juu” Alisema Jafo.
Akitaja sababu zilizochelewesha ujenzi wa Hospital ya Uhuru Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Mhe. Belnith Mahenge amesem michoro ya Hospital imechelewa kupatikana na zaidi fedha zilizoelekezwa hazijaingia kwenye Akaunti husika ili ziweze kutumika kwenye ujenzi.
Aidha Rc Mahenge alimshkuru Waziri Jafo kwa ziara yake na kusema maagizo yote
yaliyotolewa yamepokelewa na yatatekelezwa; Ujenzi wa Hospital ya Uhuru utaanza
mara moja.
Ujenzi wa Hospital ya Uhuru ni Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa mwezi Dec, 2018 ambapo aliagiza
shilingi bil. 900 zilizokuwa zitumike kwenye sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa
Tanzania zitumike kujenga Hospital Kisasa Mkoani Dodoma na kuongezafedha zaidi
shilingi Bil 2.5 kutoka katika Gawiwo lililotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel.