Na Mwandishi wetu Dodoma

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), limeipatia Serikali ya Tanzania msaada wa vifaa vya kusimamia huduma za dharura wakati wa maafa ilikuimarisha uwezo wananchi katika kukabiliana na maafa nchini.

Akipokea msaada huo leo Oktoba 25, 226, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, James Kilabuko, ameishukuru (WFP) na kueleza kuwa Serikali inaendelea kujiimarisha katika mifumo ya kitaifa ya maandalizi na muitikio wa maafa hasa katika kusimamia na kusambaza vifaa vya maafa kwa wakati.

Dkt. Kilabuko amesema msaada wa maghala sita ya kuhamishika yenye ukubwa wa mita za mraba takribani 2400 na uwezo kuhifadhi tani 800 pamoja na paleti 1000 (vifaa vya plastiki vinavyotumika kuhifadhi mizigo) kutoka shirika hilo, yatasaidia kuimarisha mpangilio wa uhifadhi wa mzigo.

“Maghala hayo ya kuhamishika yatasambazwa katika mikoa minne ya kipaumbele ambayo ni Kigoma, Kagera, Ruvuma na Tanga ikiwa ni moja ya hatua za kusaidia kusogeza huduma karibu na kuimarisha uwezo wa kujiandaa kukabiliana na maafa,” alieleza Naibu Katibu Mkuu.

Msaada huu ni kielelezo cha ushirikiano uliopo kati ya Serikali na (WFP) katika kuimarisha mifumo ya kitafa ya maandalizi ya ya kukabiliana na maafa.

Dkt, Kilabuko amelishukuru shirika la World Food Program (WFP) kwa msaada huo muhimu lililoipatia Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao unalenga kuimarisha uwezo wa kukabiliana na kusimamia maafa.

Awali, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Brigedia Jenerali, Hosea Ndagala, ameishukuru (WFP) kwa msaada wa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kuongeza nguvu katika maghala ya kimkakati yaliyoo kwenye kanda sita nchini.

Maghala hayo yatasaidia kupunguza umbali na muda kutoka kwenye maghala ya kanda na kufika eneo lenye uhitaji wa msaada wa dharura wa maafa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa (WFP), Bi, Christine Mendes, amesema vifaa walivyotoa ni vifaa himilivu kwa mazingira yote ya joto na baridi na viko katika mazingira mazuri ya utendaji wa kazi.

“Tumelenga kupeleka maghala manne ya kuhamishika katika mikoa ya Kigoma, Kagera Tanga na Ruvuma na mawili yatabaki Jijini Dodoma kwa huduma za dharura zitakazojitokeza.” Bi, Mendes.

Amesema (WFP) imetoa mafunzo ya kujengeana uwezo katika dharura kwa wataalamu wa Idara ya Menejimenti ya Maafa ambayo yamewawezesha kupata ujuzi wa kufunga na kutumia kwa ufanisi maghala ya kuhamishika.