Benki ya NMB imetangaza washindi 20 wa kwanza wa kampeni yake ya Bonge la Mpango ‘Weka na Ushinde’, inayolenga kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa Watanzania. Washindi hao wametangazwa kufuatia droo iliyofanyika jana katika Soko la Mwanjelwa, jijini Mbeya, ambapo kila mmoja amejishindia Sh 100,000.
Akizungumza wakati wa droo hiyo, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Wogofya Mfalamagoha, alisema benki hiyo imetenga Sh milioni 600 kwa ajili ya zawadi mbalimbali kupitia kampeni hiyo, inayolenga kuwajengea wateja nidhamu ya kuweka akiba ili kufikia malengo yao ya kifedha.
Mbali na zawadi za fedha taslimu za Sh 100,000 kwa kila mshindi wa droo za kila wiki na Sh 500,000 kwa kila mshindi wa droo za kila mwezi, wateja wana fursa ya kujishindia pikipiki 20 (bodaboda) na magari matatu mapya, yakiwemo mawili aina ya Ford Ranger na Toyota Land Cruiser moja maalumu kwa shughuli za utalii.
Kampeni hiyo, itakayohitimishwa Januari 31, 2027, inawahamasisha wateja wa NMB kuweka akiba kwa malengo huku wakipata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali. Droo za kampeni hiyo zinafanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.
#NMB #BongeLaMpango #WekaNaUshinde

