Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko
huo, Dkt. Abdulsalaam Omary(kulia), akikabidhi sehemu ya vifaa hivyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu MOI, Dkt. Respisious Biniface wakati wa hafla hiyo Juni 19, 2019.
Picha ya pamoja baadhi ya wafanyakazi wa WCF na wafanyakazi wa MOI katika Wiki ya Utumishi wa Umma,
Wafanyakazi wa WCF wakiwa katika zoezi la usafi katika eneo la MOI
Dkt. Omary akitoa somo kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), kwa baadhi ya watumishi wa MOI ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uytumishi wa Umma Juni 19, 2019
**********************
NA EMMANUEL MBATILO
Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa wanyakazi WCF wametoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya milioni 5 katika taasisi ya tiba ya mifupa, upasuaji wa mgongo na mishipa ya fahamu MOI kwaajili ya kujikinga na kutoa tiba kwa wagonjwa wa ajali pamoja na kujikinga na ajali ndogondogo zinazojitokeza mara kwa mara utoaji huduma.
Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa huduma za tathimini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary amesema kuwa katika wiki hii ya utumishi wa Umma wameona ni bora wao waweze kujitoa kuhakikisha kwamba wanaenda katika jamii na kusaidia mpaka pale wanapoona inawezekana.
Tunatambau serikali imeweka nguvu kubwa katika kuboresha masuala ya afya katika hospitali mbalimbali kwaqhiyo sis leo tumeamua kuchangia vitu vichache ili kuweza kuisapoti serikali katika nia yake njema ambayo mpaka sasa hivi imekuwa ikiendelea nayo”. Amesema Dkt. Omary.
Aidha Dkt. Omary amesema wataendelea kushiriki kufanya usafi katika eneo la MOI na vilevile katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi wameanzisha dawati la malalamiko ambapo watakuwa wanapokea malalamiko kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 11 wananchi wote ambao watataka kupeleka maoni au malalamiko wanawakaribisha katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa MOI, Dkt. Respicious Boniface amewashukuru wafanyakazi hao kwa kuweza kuwaletea msaada huo kwasababu utasaidia kutoa tiba kwa wagonjwa wanaowapokea na kuwatibu.